NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Tuesday, March 12, 2013

MREMBO AUAWA KINYAMA

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
DADA mmoja anayedaiwa kuwa mkazi wa jijini Dar es Salaam ameuawa kinyama baada ya kubakwa hadi kufa eneo la Nanenane ndani ya mashamba ya mikonge mjini hapa.

Mrembo baada ya kuuawa.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, mrembo huyo ambaye hakufahamika aliuawa kwa kubakwa na watu wasiojulikana ambapo maiti yake ilikutwa ikiwa imevuliwa nguo za ndani
Aidha, kwenye shingo yake kulikutwa na kitambaa ambacho inadhaniwa kuwa ndicho kilichotumika na wahalifu kumnyongea.
Baada ya polisi kukagua pochi yake walikuta ikiwa na tiketi iliyoonyesha kuwa alisafiri kutoka Dar es Salaam hadi mjini hapa bila kuwa na jina la msafiri.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia maiti hiyo, wamesikitishwa na tukio hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustene Shilogile alipohojiwa juzi na mwandishi wetu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Nawaomba watu wanaomfahamu marehemu huyu wafike chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kumtambua,” alisema Shilogile.

Tuesday, March 5, 2013

NDOA YA MONALISA KUVUNJIKA, SIRI NJE

Stori: Imela Mtema
SIRI ya kuvunjika kwa ndoa ya staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa’ imevuja ambapo imeelezwa kuwa tattoo aliyokuwa ameichora mkononi mwake yenye alama ya kopa na mshale ndiyo chanzo.
Akizungumza na Tollywood Newz jijini Dar es Salaam, Monalisa alisema: “Sikuwahi kuwaza hili hata mara moja. Siku moja Kanisani, Mchungaji aliniambia kwamba tattoo yangu ndiyo chanzo cha kunivurugia uhusiano wangu.
“Aliniambia kwamba, alama ya kopa ambayo humaanisha moyo – upendo, halafu mshale kupita katikati yake, humaanisha maumivu na kuteswa katika uhusiano. Lilikuwa jambo jipya kwangu lakini niliamua kufuta haraka sana na sasa nimeweka nyingine ya ua rose.”
Stori: Imela Mtema SIRI ya kuvunjika kwa ndoa ya staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa’ imevuja ambapo imeelezwa kuwa tattoo aliyokuwa ameichora mkononi mwake yenye alama ya kopa na mshale ndiyo chanzo.
Akizungumza na Tollywood Newz jijini Dar es Salaam, Monalisa alisema: “Sikuwahi kuwaza hili hata mara moja. Siku moja Kanisani, Mchungaji aliniambia kwamba tattoo yangu ndiyo chanzo cha kunivurugia uhusiano wangu.
“Aliniambia kwamba, alama ya kopa ambayo humaanisha moyo – upendo, halafu mshale kupita katikati yake, humaanisha maumivu na kuteswa katika uhusiano. Lilikuwa jambo jipya kwangu lakini niliamua kufuta haraka sana na sasa nimeweka nyingine ya ua rose.”

POLISI WAMWEKA KATIKATI RAY C

-KISA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA
Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
ILI kuhakikisha harudi tena kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, jeshi la polisi nchini, limemweka kati mwanamuziki Rehema Yusuf Chalamila ‘Ray C’.
Rehema Yusuf Chalamila ‘Ray C’.
Kamanda wa jeshi la polisi, kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini, Godfrey Nzowa, amesema kuwa Ray C kila anapotembea anakuwa katikati ya askari wanaofuatilia nyendo zake.
“Kila anapokwenda, askari wamemzunguka. Tangu alipopata nafuu, tumekuwa tukihakikisha havutiwi na makundi mabaya, vilevile tunataka kuona kweli amejirekebisha,” alisema Nzowa na kuongeza:
“Ray C mwenyewe haoni lakini kila anapotoka, askari wanamuweka katikati. Kwa kifupi kipindi hiki tumemuweka katikati yetu, kwani hata anapokuwa nyumbani, tunachunguza nani anaingia na anapeleka nini.”
Nzowa aliongeza kuwa kitengo chake kimeamua kumuweka kati Ray C kwa sababu mbili, moja ikiwa kubaini na kuwanasa wauzaji wanaomharibu mwanamuziki huyo, pili ni kufuatilia kama msaada uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete umefanya kazi yake ipasavyo.
“Mheshimiwa (JK) alitoa msaada wa matibabu kwa Ray C kwa nia njema, vilevile dada huyo aliapa mbele yake kama hatarudia tena. Sasa ni lazima kufuatilia na kudhibiti asije kuingia kwenye vishawishi, akakiuka kiapo na matokeo yake alichokifanya mheshimiwa kikaonekana hakina maana,” alisema Nzowa.
Kwa upande mwingine, Nzowa alisema, hali ya Ray C inaendelea kuimarika na akaongeza: “Akili yake imetulia, anaweza hata kutunga nyimbo tofauti na alivyokuwa. Watu ambao anafungamana nao kwa sasa ni wazuri, siyo magenge ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.”
Ray C, alisharipotiwa kuwa na hali mbaya baada ya kutopea kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya.
Hata hivyo, JK aliamua kujitolea kunusuru maisha ya mwanamuziki huyo kwa kugharamia matibabu yake mpaka apone.
Takriban miezi mitatu iliyopita, Ray C alitinga ikulu na kumshukuru JK kwa msaada aliompa, vilevile akawaambia Watanzania kwamba sasa anajisikia amepona na anaweza kufanya kazi.

Monday, February 25, 2013

MASTAA WA KIKE BONGO; KUTAFUTA USTAA, FEDHA KUTAWADHALILISHA SANA TU!

UPENDO ndiyo dini yangu! Ndiyo maana natumia safu hii kuwarekebisha mastaa wetu ili nitii matakwa ya dini yangu yaani kuwapenda! Hakuna ubishi kuwa umaarufu ni gharama. Ni ghali. Wakati mwingine husababisha kubadili maisha halisi ili kufikia lengo. Ikiwezekana kuondoa utu kwa kujitoa fahamu na kufanya mambo ya kujidhalilisha. Ndivyo ilivyo kwa wasanii wetu. Imewabidi kuishi maisha ya kuigiza ili kujitwalia umaarufu.
Aunt Ezekiel.
Ili kupata umaarufu ni lazima uwe na fedha. Itakubidi ujue sehemu za kwenda kubadilisha mawazo na kustarehe na mastaa wenzako. Siyo sehemu za bei rahisi. Mara nyingi kama staa akijishusha sana, ni kwenye migahawa kama ile ya pale Mlimani City, Dar.
Hawali vyakula vya ovyo. Ni baga na ‘take away’ za gharama. Siyo chipsi vumbi. Hawapandi usafiri wa jumuiya (public transport). Unachezea ustaa wewe?
Ili kukidhi matakwa tajwa hapo juu uitwe staa inawalazimu kutafuta fedha kwa njia yoyote ile ili kugharamia ustaa. Hilo ndilo lililowaponza mastaa wa kike Bongo. Kwa kuwa hawana vipato na wanahitaji maisha ya kujiachia kwenye kumbi za starehe usiku na kulala mchana kutwa, imewabidi kutumia miili yao. Ni kwa kujiuza na kuuzwa kwa wanaume kutoa huduma ya ngono ili kujipatia fedha za kushikilia ustaa. Ama kweli kusaka umaarufu kumewafanya dada zetu kuwa watumwa wa ngono.
Ipo mifano lukuki kwa mastaa walioamua kuwaacha wanaume waliokuwa nao kabla hawajapata umaarufu na kukimbilia kuolewa na watu wenye fedha.
Wolper.
Hata hivyo, kwa kuwa walifuata fedha na siyo mapenzi kwa wanaume hao, walipoishiwa na mapenzi yaliisha. Ndoa ziliota mbawa.
Wapo mastaa wa kike walioshindwa kudumu kwenye ndoa kwa kuwa wanaume waliowaoa waliishiwa na pesa.
Iko wapi ndoa ya kifahari ya Irene Uwoya? Kuna madai kuwa baada ya mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kuishiwa fedha, ndipo dada yetu akazingua.
Unakumbuka ndoa ya kifahari ya Jacqueline Patrick na Abdullatif Fundikira? Ilielezwa kuwa baada ya jamaa huyo kutupwa selo katika Gereza la Keko, Dar kwa kisanga cha mihadarati, Jack alichukua hamsini zake, akijua kabisa kwamba mkwanja umeota mbawa. Hakuwahi kwenda kumuona selo kudhihirisha kuwa hakuwa na mapenzi ya dhati na mumewe huyo bali alifuata mkwanja.
Unakumbuka penzi la Jacqueline Wolper na Abdallah Mtoro ‘Dallas’? Inasadikiwa kuwa baada ya fedha za mshikaji huyo aliyekuwa amemnunulia Wolper gari aina ya BMW X6 kurudi kwao ndipo sistaduu huyo akakata mguu na kusitisha uchumba wao.
Unajua anayempa Wema jeuri ya kubadili magari kama nguo, kutamba kununua nyumba ya mamilioni na kufungua ofisi ya kifahari? Inaelezwa kuwa ni mume wa mtu anayetajwa kwa jina la Clement au CK, kigogo katika idara nyeti nchini.
Aunt Ezekiel ameolewa na Sunday Demonte, jamaa mwenye mkwanja mbuzi ambaye hata hivyo hawaishi wote. Aunt yupo Bongo akisubiri kutumiwa fedha ya matumizi na bwana huyo aliyeko Dubai.
Hivi karibuni Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ alinaswa na mapaparazi wa Global akiuzwa kwa dola 500 akafanye ngono na mwanaume aliyejifanya Mtanzania aishie Marekani. Ni aibu lakini atafanyaje ili kukidhi vigezo vya ustaa? Lazima awe na fedha kwa njia yoyote. Ipi? Kukubali kuuzwa kingono.
Nimetoa mifano michache mno lakini ni mingi. Ukweli ni kwamba hali ni mbaya. Wasipobadilika, wataendelea kudhalilika sana tu kabla ya madhara mengine ikiwemo kuambukizwa magonjwa hatarishi hasa Ukimwi. For the love of game!

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ BACK TO SCHOOL

AJIPANGA KURUDI DARASANI UPYA!
Ni takriban mwezi mmoja tangu staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ au ‘Lizy’ alipopata dhamana na kurejea uraiani akiwa amesota katika mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar karibia miezi kumi, akikabiliwa na shitaka la kumuua bila kusudia mwigizaji Steven Kanumba.

BACK TO SCHOOL
Akiwa uraiani akisubiri kesi yake kuendelea kuunguruma, Lulu sasa anajipanga kurejea darasani kujiendeleza na masomo (back to school) kwa mara nyingine.
Habari za ndani zilieleza kuwa lengo ni kumwezesha staa huyo mkali mbele ya kamera za Bongo Movies kupambana na changamoto za kimaisha.
Habari hizo za uhakika zilieleza kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo ya sekondari aliyokuwa amesimama kwa muda.
AKWAMA, KISA?
Pamoja na kwamba mkakati huo unaendeshwa na familia, habari hizo zilidai kuwa suala kubwa linalokwamisha program hiyo kwa sasa ni kipato.
Habari za chini zilidai kuwa familia kwa sasa haina uwezo wa kumlipia shule za gharama kubwa na badala yake anatakiwa kuanza kufanya kazi ili ajikwamue katika hilo.
KUCHANGAMKIA TENDA ZA FILAMU
Ilifahamika kuwa kazi ambazo zitamwingizia mkwanja mrefu ili kumudu gharama za masomo yake na mdogo wake kama ilivyokuwa awali ni kuchangamkia tenda za filamu kutoka kwa watu mbalimbali ambazo kwa bahati nzuri tayari zimejitokeza.
Pia ilifahamika kuwa mbali na kusoma na kusomesha, alikuwa akilipa kodi ya nyumba na mambo mengine ya kifamilia hivyo atarejea kule kwa awali.
NENO LA DK. CHENI
Kwa mujibu wa mwigizaji mkubwa ambaye ni mtu wa karibu wa familia ya Lulu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, kurudi shuleni kwa staa huyo ni jambo jema ili aweze kujikwamua kielimu na kupambana na maisha ili kufanikisha malengo aliyojipangia.
Hakuna ubishi kuwa kurejea darasani kwa Lulu ambaye bado ni mdogo kiumri ni nafasi pekee ya kufanikisha malengo yake hata kama ni sanaa ambaye akishapata elimu ataifanya kisomi zaidi.
KWA NINI ALIACHA SHULE?
Kabla ya kukutwa na mashaibu, Lulu alipitia shule mbalimbali za sekondari kabla ya kusimama kumaliza au kuacha masomo akiwa kidato cha nne katika Sekondari ya Perfect Vision iliyopo Ubungo, Dar lakini sababu za kufanya hivyo hazikupatikana.

RAY AKONGOROKA


Stori: Musa Mateja na Imelda Mtema
MWIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ amezua hofu kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake baada ya kukongoroka ghafla akihisiwa anaumwa, Ijumaa Wikienda limemfuatilia hatua kwa hatua.
Vincent Kigosi ‘Ray’ alivyo kwa sasa.
KWENYE ‘BETHIDEI’ YA BATULI
Wiki kadhaa zilizopita paparazi wetu alishtuka alipomuona Ray kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji sistaduu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ndani ya Hoteli ya Shamoll iliyopo Sinza ya Lion, Dar akiwa amekongoroka na kuibua maswali kwa wahudhuriaji.
Akiwa ukumbini hapo, minong’ono ilienea kuwa Ray alionekana kukondeana katika kipindi kifupi huku baadhi ya watu wakisikika wakiulizana kulikoni kwani alikuwa meza moja na bonge la mtu, Jacob Steven ‘JB’ hivyo kumfanya kuonekana mdogo mno.
Vincent Kigosi ‘Ray’ alivyokuwa mwaka jana.
VIWANJA VYA LEADERS
Akiwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki iliyopita, Ray aliibua mshtuko kwa mara nyingine hadi jamaa mmoja anayedhaniwa kutokuwa vizuri kichwani kumfuata na kumuwakia akimuuliza kwa hasira kuwa kulikoni akondeana kiasi hicho.
UZINDUZI WA WEMA
Kwa mara nyingine, Ray alizua hofu alipohudhuria kwenye uzinduzi wa ofisi ya Wema Sepetu uliofanyika maeneo ya Kinondoni, Dar ambapo alipoingia watu walipigwa butwaa wakimtazama na wengine kumuonea huruma wakidhani anaumwa.
IJUMAA WIKIENDA LATAKA MAJIBU
Kwa nyakati tofauti, wanahabari wetu walizungumza na Ray ambaye alitoa majibu ya kukinzana na kuzidi kutia shaka.
Ray alimwambia mmoja wa waandishi wetu kuwa kilichosababisha akongoroke kiasi hicho ni mazoezi makali anayofanya ili kupunguza unene.
Katika majibu mengine kwa mwandishi wetu mwingine, Ray alidai kuwa anafanya ‘dayati’ ikielezwa kuwa ikishafika saa 11:00 jioni ndiyo mwisho wake wa kula msosi lengo likiwa ni kupunguza mwili uliokuwa umefumuka.
Kama mtu alimuona Ray kwenye Matamasha ya Serengeti Fiesta mwishoni mwa mwaka jana, akikutana naye lazima amtazame mara mbilimbili hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni kutafuta undani wa madai kuwa huenda staa huyo mkubwa anaumwa kufuatia majibu tofauti aliyoyatoa.