NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, March 29, 2013

RECHO: SINA UHAKIKA WA KUOLEWA NA SAGUDA

Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Rachel Haule ‘Recho’ amefunguka kuwa japokuwa wamekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mpenzi wake George Saguda bado hana uhakika kama ndiye atakayemuoa.
Akichonga na paparazi wetu, Recho alisema kuwa kutoka moyoni anampenda Saguda na anatamani siku moja awe mume wake ila kufanikiwa wao kuoana anamuachia Mungu kwani ndiye anayepanga kila jambo
 “Suala la ndoa namuachia Mungu kwa sababu wapo mastaa wengi waliochumbiwa lakini wameishia kuzalishwa na kuachwa hivyo mimi naamini kama Mungu amenipangia Saguda awe mume wangu atanioa lakini kama siyo basi siwezi kulazimisha,” alisema Recho.

Thursday, March 28, 2013

UNAPOPATA FEDHA, ‘USIZITUMBUE’ KANA KWAMBA KESHO HAIPO!


Leo nataka kuzungumzia tabia ya baadhi ya watu kutumia fedha wanazozipata kwa fujo kana kwamba wameambiwa kuwa kesho wanakufa. Hakuna asiyefahamu umuhimu wa pesa, na kutokana na hilo, wengi wamekuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha wanazipata.
Cha ajabu sasa, wapo ambao wanatumia nguvu na akili zao kuzitafuta fedha hizo lakini mwishowe wanazimwaga kwa matumizi yasiyo na mbele wala nyuma.
Utakubaliana na mimi kwamba wapo watu ambao leo hii wanashinda wakibeba zege, kuzibua mitaro, kubeba mizigo na kazi nyingine nzito lakini jioni wanapopata ujira hukimbilia baa na kuzitumbua kwa staili ya lete kama tulivyo.
Ninachokizungumza kipo huko mtaani, watu wanatumia pesa kama vile wana uhakika wa kuendelea kuzipata kila siku. Ndiyo maana nadiriki kusema kwamba kutumia pesa ovyo ni sawa kabisa na kujiandalia ufukara wa baadaye.
Wapo watu wengi tu ambao kwa sasa ni mafukara wa kutupwa lakini utakapojaribu kuangalia historia yao huko nyuma utagundua walikuwa na pesa nyingi ila walikuwa wakizutumia kana kwamba wanamkomoa mtu lakini leo wanaishi maisha ya kuungaunga, hawana mwelekeo.
 Sikatai kwamba matumizi ya mtu yanatokana na kipato chake na ndiyo maana mtu anayepokea mshahara wa shilingi milioni moja kwa mwezi hawezi kuwa na matumizi sawa na mtu anayepokea laki moja lakini je, kuwa na kipato kikubwa ndiyo kukufanye utumie fedha zako ovyo eti kwa sababu tu una uhakika wa kupata nyingine mwezi ujao?
Jamani tukumbuke kwamba, maisha ni kupanda na kushuka. Leo hii unafanya kazi katika kampuni ama shirika fulani lakini uwezekano wa kuwepo katika shirika hilo kwa kipindi chote cha maisha yako ni mdogo. Unaweza kuachishwa kazi wakati wowote.
Sasa kama ulikuwa unatumia ovyo pesa uliyokuwa unaipata, unatarajia nini kama siyo kuingia kwenye ufukara ambao kwa kiasi fulani ungeweza kupunguza ukali wake kama ungekuwa makini katika matumizi ya pesa zako?
Utumiaji ovyo wa pesa ni kuzitumia bila mpangalio tena wakati mwingine katika mambo ambayo si ya msingi lakini tutambue kwamba, ufujaji wa pesa hauko katika anasa tu kama vile ulevi, kuhonga na mambo mengine kama hayo, bali pia katika mambo ambayo hata yakikosekana hayawezi kuleta athari.
Tafiti mbalimbali zimeonesha kwamba, wengi ambao hutumia pesa ovyo ni athari za malezi waliyoyapata kutoka kwa wazazi wao tangu utotoni. Mzazi ndiye anayeweza kumfundisha mtoto wake kutokuwa na nidhamu katika pesa.

Itaendelea wiki ijayo.

Thursday, March 21, 2013

HAWA NDIYO... ‘WATAALAM’ WA PICHA ZA UTUPU BONGO


Makala na Erick Evarist
NCHI za wenzetu staa kupiga picha za utupu si kitu kigeni lakini Kibongobongo sheria na maadili ya Mtanzania hayaruhusu kufanya hivyo.
Licha ya kubanwa na sheria pamoja na maadili, wapo wasanii ambao kwa nyakati tofauti walijikuta katika adha ya kupigwa kama si kujipiga picha za utupu kisha zikazagaa mitaani.
Wapo waliotajwa kupiga picha hizo kwa kusaka umaarufu, waliopigwa na wapenzi wao kisha wakazivujisha lakini wengine imedaiwa kuwa wamezivujisha wenyewe na kusingizia zimevujishwa na wapenzi wao.
Ifuatayo ni orodha ya wasanii mbalimbali Bongo ambao waliwahi kukwaa skendo ya picha za utupu:
Wema Sepetu:
Mwaka 2010 picha yake ya utupu ilizagaa mtandaoni huku ikidaiwa kuwa chanzo cha kusambaa kwake ni boifrendi wake ambaye alimpiga na kuzisambaza. Kama hiyo haitoshi, mwaka huu mrembo huyo alidaiwa kuposti picha zake nyingine za utupu katika mtandao wa Instagram.
Diana Hussein:
Huyu  ni Miss Dar Indian Ocean ambaye pia ni Miss Kinondoni namba 2 mwaka jana, mrembo huyo hivi karibuni amejikuta akipata aibu baada ya picha yake ya utupu kuvuja. Ilidaiwa kuwa alifanya hivyo kwa azma ya kusaka umaarufu.
Jack wa Chuz:
Ni bonge la ‘actress’ Bongo Movie, mwaka 2012 alipigwa picha za utupu na kusambazwa kila kona ya Jiji la Dar. Ilidaiwa kuwa kuna mtu alizichukua picha hizo kutoka kwenye simu yake na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari.
Agness Masogange:
Nini picha! Yeye ilivuja video yake ya utupu kabisa. Ilisambaa kama njugu katika mitandao ya kijamii mwaka jana. Vyanzo makini vilidai kuwa video hiyo alipigwa na mpenzi wake na haikujulikana mara moja chanzo kilichozivujisha.
Jacqueline Wolper:
Pamoja na heshima kubwa aliyonayo kwenye soko la filamu, mapema mwaka huu staa huyo amejikuta akichafuka baada ya picha yake ya utupu kuanikwa gazetini. Ilidaiwa kuwa picha hiyo alipigwa kwenye bethidei ya msanii mwenzake.
Marry John:
Msanii wa filamu Bongo, Mary John ‘Maua’ mwaka jana alijipatia jina baada ya kupiga picha kadhaa za utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii yeye mwenyewe.
Aunt Lulu:
Mara kadhaa amekuwa akitengeneza vichwa vya habari magazetini kwa kupiga picha za utupu. Mfano hai ni picha ambazo alipiga mwaka jana, ambapo alidai kuwa alipigwa bichi alipokwenda ‘kula bata’.
Lulu:
Mwaka 2010 alijikuta akichafuka kwa kutajwa kwenye skendo ya kupiga picha ya utupu. Alipoulizwa kuhusiana na picha hiyo alikanusha kuwa si ya kwake na kudai kuwa ilitengenezwa na watu ili kumchafua.
Jack Patrick:
Kwa upande wake suala la kuvuja kwa picha zake za utupu siyo ishu. Mwaka jana ilidaiwa kuwa aliziposti picha zake za utupu kwenye mtandao wa BBM, haileweki ni kwa nini huwa anafanya hivyo.
Isabela ‘Vai wa Ukweli’:
Huyu ni chipukizi kwenye anga la filamu Bongo, mara kadhaa amepigwa picha za utupu na kusambazwa kwenye vyombo vya habari. Imedaiwa kuwa hufanya hivyo kama kutafuta mlango wa kutokea kwenye ustaa.
Maadili ya Mtanzania yanatukataza kufanya vitendo vya namna hii hivyo ni vyema wahusika wakawa makini, waepuke kupiga wala kuhusika kusambaza picha zao za utupu kwa namna yoyote ile.      

UKATILI 100%

Na Patrick Mabula, Kahama
HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake, Amani lina habari ya kusikitisha.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Asack Nzolela (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.
Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja  mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia.
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.
Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.
Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.
Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.
Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19).
Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na gazeti hili alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzolela katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzolela amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.
Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.

Friday, March 15, 2013

WAGANGA 12 KUMTIBU JAY DEE

Na Hamida Hassan
WAGANGA wanaodai kuwa ni wataalam na wana uzoefu wa kupambana na jini mahaba linalomsumbua Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, wamejitokeza huku kila mmoja akiomba apewe nafasi ya kumtibu bure.
Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’.
Baada ya gazeti hili toleo lililopita kuingia mtaani na stori inayoeleza jinsi jini mahaba anavyomsumbua Jide, watu wapatao 12 waliojitambulisha kuwa ni wataalam wa mambo hayo waliomba kuunganishwa na mke huyo wa Mtangazaji wa Radio Times FM, Gardner G. Habash huku wakiahidi kumtibu bila gharama yoyote.
Mmoja wa wataalam hao aliyejitambulisha kwa jina la Jumaa wa Magomeni, Dar alisema: “Nimesoma habari kuhusu Jide, mimi naweza kumtibu tena bure, mpe namba yangu na mwambie anipigie.”
Mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema: “Nimesikitika sana kusoma hii habari ya huyu msanii Lady Jaydee, kwa kifupi naweza kumtibia free of charge.”
Kufuatia maombi ya wataalam hao, mwandishi wetu alijitahidi kumtafuta Jide bila mafanikio lakini juzikati kupitia kipindi chake cha Diary ya Lady Jaydee alionekana akipewa matibabu na ustaadhi mmoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda mambo yametulia.

KHADIJA YUSUF AJIFUNGUA, MTOTO AFARIKI TENA!

Na Mwaija Salum
KWA mara nyingine tena, mwimbaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab la jijini Dar, Khadija Yusuf amejifungua na mtoto kufariki dunia, Ijumaa limetonywa.
Khadija Yusuf.
Habari hizi za masikitiko zimepokelewa katika chumba chetu cha habari Jumatano iliyopita na kuthibitishwa na wadau wa mbalimbali wa muziki wa taarab.
“Khadija amejifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini mtoto si riziki,” amesema mmoja wa wadau wa muziki huo.
Mwanzoni mwa mwaka jana, mwimbaji huyo aliyewahi kuimbia makundi ya The East African Melody, Zanzibar Stars na Five Stars alijifungua kwa upasuaji baada ya kusumbuliwa na presha lakini mtoto alifariki dunia.
Hii ni mara ya tatu kwa Khadija kupoteza watoto katika uzazi, mwaka jana alipewa onyo na daktari kwamba asishike mimba mpaka baada ya miaka mitatu lakini hakutii agizo hilo.

Thursday, March 14, 2013

DENTI ALIYEPIGA PICHA ZA UTUPU ADAIWA KUTENGWA NA FAMILIA

Na Mwandishi Wetu
YULE denti wa chuo kimoja jijini Mwanza ambaye wiki iliyopita tuliandika habari ya picha zake za utupu kuzagaa kwenye mtandao wa BBM, Fatuma Omari amejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia madai kuwa familia yake imemtenga.
Denti Fatuma Omari akiwa katika pozi.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, mara baada ya kutoka kwa habari hiyo, baadhi ya ndugu zake walikasirika na  kutaka kujua undani wake.
“Ile stori ilipotoka ndugu wa Fatuma hawakuamini kuwa kweli kapiga picha hizo.
“Kwa bahati kuna mtu aliyekuwa na picha hizo, walipoziona, waliumia sana na baadhi wakafikia hatua ya kusema hawana radhi naye,” kilidai chanzo hicho.
Ijumaa lilimtafuta Fatuma ili kuzungumzia madai hayo bila mafanikio ila kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Saleh baada ya stori kutoka, alilipigia simu Ijumaa na kusema:
“Fatu ni mdogo wangu, nashangaa mmemuandika kuwa kapiga picha chafu wakati siyo kweli. Kama hizo picha zipo nitakuja kuziona laa sivyo tutapelekena mahakamani,” alisema Saleh.
Tumeamua kutumia picha hiyo chafu hapo chini aliyopiga Fatuma ili kuonesha uhalisia.