NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Saturday, April 27, 2013

DENTI WA CHUO KIKUU ARUSHA ALIVYOUAWA


Stori:Joseph Ngilisho,Arusha
MWANAFUNZI wa mwaka wa pili  katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini hapa, Henry Koga, ameuawa kikatili na hivi ndivyo alivyouawa.
Enzi za uhai wa mwanafunzi huyo
Kwa mujibu wa wanachuo wenzake ambao hawakutaka majina yao kuandikwa gazetini, Koga aliuawa kinyama kwa kuchomwa kisu shingoni na kundi la watu wasiofahamika wakati akitoka kujisomea nje ya chuo usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Imeelezwa kuwa tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo lilitokea saa 4 usiku ambapo marehemu huyo akiwa na wenzake walivamiwa na kundi la wahuni wapatao wanne katika eneo la CDA, jirani na chuo hicho na Koga kuchomwa kisu shingoni na kifuani.
Wanachuo wenzake walisema marehemu hakuwa anatoka kwenye starehe kama watu wengine wanavyodai bali alikuwa na wenzake  wakitoka kujisomea nje kidogo ya chuo hicho kwa ajili ya kujiandaa na mitihani na walipofika eneo hilo, wakavamiwa na watu wasiojulikana.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wanafunzi  walijikusanya asubuhi yake na kuanza kuandamana kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutoa tamko juu ya vitendo vya uhalifu vinavyojirudia mara kwa mara chuoni hapo.
Kufuatia tukio hilo, wanachuo hao walifanya vurugu kubwa na kumlazimisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kwenda chuoni hapo, alipofika kulitokea hali ya kutoelewana ambapo walimzomea na kumpiga mawe, hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuwafyatulia mabomu ya machozi.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema naye alijitahidi kuwatuliza bila mafanikio huku ikidaiwa yeye ndiyo chanzo cha vurugu hivyo kutakiwa kukamatwa. Mkuu wa mkoa alilazimika kuondoka eneo kuokoa maisha yake.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Ibrahimu Kilongo akizungumzia tukio hilo, alisema wanachuo 10 wanashikiliwa na polisi kutokana na vurugu hizo na kwamba uchunguzi unaendelea.

Wednesday, April 3, 2013

PICHA 5 ZA LAANA YA "KANGA MOJA" KATIKA SHOW YA MSANII DIAMOND- BUKOBA


Mambo yanayofanywa na kundi la kanga moja ni ya aibu sana  kwa  sababu  ni  uchafu  unaotendeka  mbele  ya  watoto......

Mwanamke  hujifunga  kanga  moja  tu  bila  chupi  wala  chochote  ndani.Baada  ya  hapo  humwagiwa  maji  kitu ambacho  huanika  kila  kitu  hadharani......

Kama haitoshi, akimwagiwa  maji, wenzie  huanza  kumtia  chupa  matakoni  hali  inayoashiria  VITENDO  VYA  ULAWITI......

Tunawafundisha  nini  watoto???..Tunaifundisha  nini  jamii  na  kizazi  cha  kesho????





Friday, March 29, 2013

USHIRIKINA!


Na Mwandishi Wetu, Mbeya
HII inasikitisha na inashangaza sana!
MWANAMKE mmoja ambaye ni mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la Atupele mkazi wa Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi, jijini hapa, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya wakazi wa eo hilo kumpa kibano wakimtuhumu kwa ushirikina.
Mama Atupele anayetuhumiwa kwa ushirikina
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni baada ya mtoto aliyetambuliwa kwa jina la Judith Chengula (3) kupotea katika mazingira ya kutatanisha, Februari 22, mwaka huu.
Kwa mujibu wa wakazi hao, mtoto huyo alipotea majira ya saa 11 jioni wakati alipokuwa akitoka kanisani na dada yake aitwaye Anitha Mgaya.
Imeelezwa kwamba, baada ya wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kumtafuta Judith bila mafanikio, walikaa vikao kadhaa lakini Atupele hakuhudhuria.
Habari zinadai kwamba, kitendo cha mtuhumiwa huyo kutohudhuria kwenye vikao hivyo kiliwapa mashaka na kuhisi huenda mama huyo anahusika na kupotea kwa Judith.
Imedaiwa kwamba Machi 23, mwaka huu asubuhi wananchi hao waliendelea kusisitiza Atupele achukuliwe hatua lakini baadaye waliamua kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alidai kuwa, baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwa mama huyo walikuta vitu vilivyodaiwa ni vitovu vya watoto wachanga, hivyo kuamsha hasira kwa raia.
“Mama huyo alipobanwa alijikuta akibabaika ndipo watu wakamvaa kabla ya kuokolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo, Nedy Mwamlima aliyempeleka polisi kwa usalama wake.
“Kwa hasira, wananchi wa aneo hilo waliingia ndani ya nyumba ya mama huyo na kutoa nje vitu mbalimbali kisha kuvichoma moto, pia walibomoa nyumba yake na kuharibu mazao yaliyokuwa nje ya nyumba hiyo,” alisema shuhuda huyo.
 Hata hivyo, gazeti hili linalaani watu kujichukulia sheria mkononi na kwamba, yanapotokea mazingira kama hayo ni vyema vyombo vya dola vikataarifiwa ili viweze kuchukua hatua sahihi badala ya kile walichokifanya wananchi wa eneo hilo-Mhariri.

KAMA UMESALITIWA, FANYA HAYA KABLA YA KUMUACHA!


Suala la wapenzi au wanandoa kusalitiana limekuwa likiwaumiza walio wengi na baadhi wanaposalitiwa hujikuta wakichanganyikiwa na wengine kuchukua maamuzi ya kukatisha maisha yao.
Hakuna anayeweza kusema kuwa, haumii anaposalitiwa na kama yupo basi huyo aliyenaye hampendi kwa dhati.
Kama unampenda, akikusaliti lazima utaumia lakini cha kujiuliza ni kwamba, tukishasalitiwa ndiyo mwisho wa maisha yetu? Tukisalitiwa na wapenzi wetu suluhisho ni kunywa sumu?
Sidhani kama hayo ni maamuzi ya busara. Yapo ya kufanya unapokumbwa na balaa hili la kusalitiwa na leo nimeona nikupe dondoo chache zinazoweza kukusaidia.
Kwanza, kubaliana na kilichotokea. Kama ameshakusaliti ni tukio ambalo limeshatendeka na huwezi kufanya chochote kulifuta. Kwa maana hiyo kubali kuwa umetendwa na kwa kuwa una moyo wa kibinadamu, huzunika mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.
Pili, usijalaumu. Kuna ambao wakishasalitiwa huanza kujilaumu ni kwa nini waliingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema; ‘Najuta kumpenda fulani’. Kujilaumu kwa namna hiyo hakutakiwi kwani kutakufanya uzidi kupata maumivu moyoni mwako na kunyong’onyea.
Tatu, jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempatia basi uchukue kisha ufanyie kazi.
Kujitoa kwako kwenye tatizo kunaweza kukupunguzia machungu kwa kiasi fulani licha ya kwamba si kazi rahisi.
Nne, je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?
Kama utapata jibu ni vyema ukachukua uamuzi ambao nafsi yako itaona ni sahihi.
Tano,usione hatari kumpasha ukweli. Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.
Sita, jaribu kuchunguza ili kujua kwa nini amefikia hatua ya kukusaliti. Usiliache likapita hivihivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.
Saba, usikubali akuletee usanii katika hilo. Nasema hivi kwa kuwa, huenda huyo mpenzi wako ni ‘mjanjamjanja’ na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia poa tukio hilo. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.
Nane, ni vyema ukachukua uamuzi sahihi. Kama amekusaliti, uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unasita, muache.
Tisa, unayo nafasi ya kumsamehe licha ya kwamba utakuwa umeachana naye. Hii itakusaidia kuliondoa dukuduku lako moyoni na kujiepusha na kukosa amani.
Kumi, chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakukuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

FLAVIANA MATATA ATUMIKA KUTAPELI MTANDAONI

Stori: Hamida Hassan
Mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata amekuwa akitumiwa na watu wasiojulikana kuwatepeli watu kupitia mtandao wa Facebook kwa akaunti yenye jina la Flaviana Matata’s huku ikidaiwa kuwa wengi wameshalizwa.
Taarifa ya Kampuni ya Compass Communications inayosimamia kazi za modo huyo inaeleza kuwa, watu hao wasiojulikana wamefungua akaunti kwenye mtandao wa Facebook na kuwarubuni watu kuwa, ‘Flaviana’ huyo anawatafutia kazi wasichana nje ya nchi kwa gharana ya shilingi hadi 200,000.
“Tunawatahadharisha watu kuwa Flaviana hatafutii wasichana kazi ya uanamitindo, wanaotumia akaunti ya Flaviana Matata’s ni genge la wahalifu, akauti sahihi ya Flaviana ni Flaviana Lavvy Matata,” ilieleza taarifa hiyo.

RECHO: SINA UHAKIKA WA KUOLEWA NA SAGUDA

Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Rachel Haule ‘Recho’ amefunguka kuwa japokuwa wamekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mpenzi wake George Saguda bado hana uhakika kama ndiye atakayemuoa.
Akichonga na paparazi wetu, Recho alisema kuwa kutoka moyoni anampenda Saguda na anatamani siku moja awe mume wake ila kufanikiwa wao kuoana anamuachia Mungu kwani ndiye anayepanga kila jambo
 “Suala la ndoa namuachia Mungu kwa sababu wapo mastaa wengi waliochumbiwa lakini wameishia kuzalishwa na kuachwa hivyo mimi naamini kama Mungu amenipangia Saguda awe mume wangu atanioa lakini kama siyo basi siwezi kulazimisha,” alisema Recho.

Thursday, March 28, 2013

UNAPOPATA FEDHA, ‘USIZITUMBUE’ KANA KWAMBA KESHO HAIPO!


Leo nataka kuzungumzia tabia ya baadhi ya watu kutumia fedha wanazozipata kwa fujo kana kwamba wameambiwa kuwa kesho wanakufa. Hakuna asiyefahamu umuhimu wa pesa, na kutokana na hilo, wengi wamekuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha wanazipata.
Cha ajabu sasa, wapo ambao wanatumia nguvu na akili zao kuzitafuta fedha hizo lakini mwishowe wanazimwaga kwa matumizi yasiyo na mbele wala nyuma.
Utakubaliana na mimi kwamba wapo watu ambao leo hii wanashinda wakibeba zege, kuzibua mitaro, kubeba mizigo na kazi nyingine nzito lakini jioni wanapopata ujira hukimbilia baa na kuzitumbua kwa staili ya lete kama tulivyo.
Ninachokizungumza kipo huko mtaani, watu wanatumia pesa kama vile wana uhakika wa kuendelea kuzipata kila siku. Ndiyo maana nadiriki kusema kwamba kutumia pesa ovyo ni sawa kabisa na kujiandalia ufukara wa baadaye.
Wapo watu wengi tu ambao kwa sasa ni mafukara wa kutupwa lakini utakapojaribu kuangalia historia yao huko nyuma utagundua walikuwa na pesa nyingi ila walikuwa wakizutumia kana kwamba wanamkomoa mtu lakini leo wanaishi maisha ya kuungaunga, hawana mwelekeo.
 Sikatai kwamba matumizi ya mtu yanatokana na kipato chake na ndiyo maana mtu anayepokea mshahara wa shilingi milioni moja kwa mwezi hawezi kuwa na matumizi sawa na mtu anayepokea laki moja lakini je, kuwa na kipato kikubwa ndiyo kukufanye utumie fedha zako ovyo eti kwa sababu tu una uhakika wa kupata nyingine mwezi ujao?
Jamani tukumbuke kwamba, maisha ni kupanda na kushuka. Leo hii unafanya kazi katika kampuni ama shirika fulani lakini uwezekano wa kuwepo katika shirika hilo kwa kipindi chote cha maisha yako ni mdogo. Unaweza kuachishwa kazi wakati wowote.
Sasa kama ulikuwa unatumia ovyo pesa uliyokuwa unaipata, unatarajia nini kama siyo kuingia kwenye ufukara ambao kwa kiasi fulani ungeweza kupunguza ukali wake kama ungekuwa makini katika matumizi ya pesa zako?
Utumiaji ovyo wa pesa ni kuzitumia bila mpangalio tena wakati mwingine katika mambo ambayo si ya msingi lakini tutambue kwamba, ufujaji wa pesa hauko katika anasa tu kama vile ulevi, kuhonga na mambo mengine kama hayo, bali pia katika mambo ambayo hata yakikosekana hayawezi kuleta athari.
Tafiti mbalimbali zimeonesha kwamba, wengi ambao hutumia pesa ovyo ni athari za malezi waliyoyapata kutoka kwa wazazi wao tangu utotoni. Mzazi ndiye anayeweza kumfundisha mtoto wake kutokuwa na nidhamu katika pesa.

Itaendelea wiki ijayo.