NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Monday, May 20, 2013

Najua Nilikukosea Sana ila Naomba Umuache Huyo Mwanamke, Amin Nitamlea Mtoto Wako Kama wa Kwangu


Hivi wanawake ni watu wa aina gani? naombeni ushauri jamani, nilikuwa na mpenzi akanisaliti akaenda kuolewa na lijibaba nikatafuta mwingine,nimezaa nae mtoto mmoja natunaishi kwa furaha.cha ajabu ameanza kunitumia mesege,mojawapo imeandikwa hivi nanukuu "Najua nilikukosea samahani sana ila naomba umuache huyo mwanamke, amin nitamlea mtoto wako kama wakwangu kumbuka unafahamika mbaka nyumbani familia yangu inanicheka kwa nilichokifanya".huyu mwanamke ninaeshi nae kaona hiyo massage kaniambia nimsamehee na yuko radhi kuondoka....Sasa nifanyaje nishaurini.

No comments:

Post a Comment