NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Saturday, January 12, 2013

Udaku Special: Baba Kanumba Atuumiwa Kutuma Watu Wakaibe Nyaraka za Mirathi ya Kanumba


BABA mzazi wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Mzee Charles Kanumba anatengeneza tena kichwa cha habari na safari hii anadaiwa kutuma watu kuiba nyaraka za mirathi nyumbani kwa mama Kanumba, Kimara Temboni jijini Dar.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake, kilidai kuwa baada ya baba Kanumba kujaribu kufungua mirathi ya mwanaye na kushindwa kutokana na kukosa viambatanisho muhimu, amekuwa akihaha kuhakikisha anavipata kwa njia yoyote.
Kikazidi kudai kuwa hivi karibuni, mzee huyo alimpigia simu mtoto wake mmoja aishiye Dar na kumtaka ahakikishe anazipata nyaraka hizo zilizopo nyumbani kwa mama Kanumba.
“Sasa hivi baba Kanumba anahaha kweli kutafuta viambatanisho muhimu vya mwanaye ili akafungue mirathi, hii ni baada ya kwenda mahakamani kujaribu kufungua bila mafanikio kwa sababu hakuwa na ushahidi wowote kuwa Kanumba ni mwanaye,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwa mama Kanumba ili kujua undani wa ishu hiyo ambapo bila hiyana mama huyo alifunguka:
“Ni kweli baba Kanumba alimpigia mtoto wake simu akimtaka afanye juu chini achukue nyaraka muhimu zinazomhusu Kanumba ambazo ni cheti cha kuzaliwa na hati ya kifo ili akafungue mirathi kwa sababu hivyo ndivyo vinamkwamisha.”
Hata hivyo, mama Kanumba alisema kutokana na maumivu aliyonayo kuhusu kifo cha mwanaye huyo, hana haraka ya kufungua mirathi kwani mwanaye hakuwa tajiri wala hana watoto watakaomsumbua.
Alipotafutwa baba Kanumba kuhusiana na sakata hilo,
 alijibu kwa kifupi: “Aache hizo. mimi sijafanya kitu kama hicho. Kuhusu mirathi nitakutajia tarehe ya kwenda mahakamani siku ikifika
Chanzo:www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment