NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Thursday, January 10, 2013

UNAKUBALI KUOLEWA NA USIYEMPENDA KISA ANA PESA, HUJITAKI?

BODABODA YAZUA BALAA KWA WAPENDANAO!


Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
MIAKA ya nyuma watu walishuhudia akina mama wakipigana vijembe kwa maneno yaliyokuwa kwenye khanga lakini sasa hali hiyo  imejitokeza kwa wanaume ambao hutumia pikipiki kuwafumbia maneno ya mafumbo watu waliokorofishana nao kwa kuyaandika katika  mipira ya ‘madigadi’.
Gazeti hili hivi karibuni likiwa kwenye duka la kuuza pikipiki lililopo Mtaa wa Mindu barabara ya kueleka Faya Manispaa ya Morogoro, lilishuhudia pikipiki nyingi zikiwa zimeandikwa ujumbe tofauti.
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sule Manga akiwa juu ya pikipiki yake iliyoandikwa maneno yanayosomeka: “Usijisifu una mimba, msifu aliyekutia mimba hiyo” alipoulizwa sababu ya kuandika hivyo alifunguka:
“Pikipiki hii nimeinunua hivi karibuni na hili pepe nililichora tangu jana nikiwa na sababu maalumu, nilikuwa na demu wangu ambaye nilimtia mimba, juzikati kaniaga anakwenda kwao Tanga, chaajabu aliporudi amekata mawasiliano na mimi huku akijisifu kwa watu kwamba ana mimba bila kunisifu mimi niliyempa mimba hiyo,” alisema Manga na kuongeza:
“Nikimpigia simu hapokei, hivyo kuanzia juzi niliamua kuachana naye kwa sasa naelekea nyumbani kwao na pikipiki hii, nikifika naipaki  jirani na nyumba yao kwa lengo la kutaka yeye na familia yake akiwemo mama yake mzazi wasome meseji hii…nasikia kambambikia mtu mwingine mimba yangu,” alisema.
Hata hivyo,  hakuwa tayari kumtaja mwanamke huyo anayedai kuwa na mimba yake. Pikipiki nyingi mjini hapa zimeandikwa maneno ya mafumbo kama yanayoandikwa kwenye khanga.


WAKATI fulani huwa najiuliza kwa nini tunakuwa na wapenzi, kwa nini mapenzi yakawepo? Kwa nini tunaoa ama kuolewa? Kwa nini baadhi ya watu huamua kujinyonga baada ya kuachwa na wapenzi wao?

Kwa nini mapenzi yameharibu baadhi ya maisha ya watu? Huwa najiuliza maswali mengi yenye kwa nini, yakihusisha mapenzi. Kwa ujumla kama nilivyo na maswali mengi, majibu pia yamekuwa mengi.
Kwa vyovyote itakavyokuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika maisha hayawezi kukamilika bila mapenzi. Ninapozungumza mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Mapenzi hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na…
WAKATI fulani huwa najiuliza kwa nini tunakuwa na wapenzi, kwa nini mapenzi yakawepo? Kwa nini tunaoa ama kuolewa? Kwa nini baadhi ya watu huamua kujinyonga baada ya kuachwa na wapenzi wao?
Kwa nini mapenzi yameharibu baadhi ya maisha ya watu? Huwa najiuliza maswali mengi yenye kwa nini, yakihusisha mapenzi. Kwa ujumla kama nilivyo na maswali mengi, majibu pia yamekuwa mengi.
Kwa vyovyote itakavyokuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika maisha hayawezi kukamilika bila mapenzi. Ninapozungumza mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Mapenzi hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo uliyemzimikia, hatari kubwa iko mbele yako.
Nasema hatari iko mbele yako najua huwezi kuwa na mwisho mzuri. Kama ni msichana utachezewa na mwisho wa siku utaachwa solemba kwa kuwa tu uliyemruhusu aingie kwenye moyo wako hajakupenda kwa dhati.
 Lakini pia kukubali kuingia kwenye uhusiano na mtu ambaye moyo wako unasema ‘no’ siku za baadaye unaweza kujikuta unachukua maamuzi ambayo yanaweza kuyaathiri maisha yako kwa kiwango kikubwa.
Kumbuka mapenzi ni nguzo ya maisha yetu tena nguzo muhimu sana. Kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utatawaliwa na amani siku zote.
Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda. Yaani yeye anaonesha kukuzimikia ile mbaya huku akikuahidi mambo mazuri lakini ukijaribu kufanya mawasiliano na moyo wako unakujibu kuwa hauko tayari kumpokea.
Ukweli wa mambo ni kwamba, mtu huyo unatakiwa kumweleza ukweli, yaani umkatalie kiroho safi tu kwa kuwa hakuna sababu za msingi za kukufanya wewe ulazimishe kuwa naye. Unalazimisha kumpenda kwa sababu za utajiri wake? Utakuwa unaidhulumu nafsi yako hivyo kwa kuwa moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, muache apite.
Muache aende kwa kuwa, penzi linaloweza kukupa amani ni lile ambalo moyo wako umeridhia. Kulazimisha penzi eti kwa kuwa umeona jamaa ana fedha za kutosha ni sawa na kujiingiza kwenye kaburi wakati bado hujafa.
Uchunguzi wangu mdogo umenionesha kuwa, kuna wasichana wengi ambao maisha yao yako gizani kwa kuwa wamekubali kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume ambao hawawapendi.
Baadhi wakitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo.
Hufanya hivyo akijidanganya kuwa eti atakuwa akiunda penzi taratibu kitu ambacho hakiwezi kufanyika na kama kitafanyika lazima usanii utakuwepo ndani yake.
Hili ni tatizo kubwa na ndiyo maana nikaona leo nilizungumzie ili kuwanusuru wale wanaohatarisha maisha yao kwa kukubali kuingia kwenye uhusiano/ndoa na watu ambao hawawapendi kwa sababu ya tamaa zao.
Kuanzi leo, kama uko kwenye uhusiano hakikisha uliyenaye unampenda na si kwamba unalazimisha kumpenda kwa sababu ya mali alizonazo. Kama hujaingia kwenye uhusiano, kuwa makini na watu wanaokutokea, unayemkubali kuwa wako hakikisha moyo wako umemuidhinisha na si vinginevyo.
Kwa leo ni hayo tu, tukutane
 wiki ijayo.

SAM WA UKWELI ADAIWA KUMTAPELI RAIS

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Salum Mohamed ‘Sam wa Ukweli’ amedaiwa kumtapeli Rais Jakaya Kikwete kwa kushindwa kutokea kwenye shoo, Gladness Mallya anashuka nayo.
Salum Mohamed ‘Sam wa Ukweli’
Kwa mujibu wa chanzo makini, Sam alifanya makubaliano na wasaidizi wa rais wakamtaka kuwa miongoni mwa wasanii ambao wangetumbuiza kwenye sherehe ya Mwaka Mpya iliyofanyika Msoga, Pwani (nyumbani kwa rais) lakini jamaa akaingia mitini.

 Baada ya kuzinyaka habari hizo, Centre Spread ilimtafuta Sam na…

TX JUNIOR ABURUZWA MAHAKAMANI

Stori: Musa Mateja

SHAROBARO wa Bendi ya Msondo Ngoma, Hassani William Moshi ‘TX Junior’, hatimaye ameburuzwa mahakamani kwa kosa la kumshambulia na kumjeruhi mrembo mmoja  anayekwenda kwa jina la Doris Elias (pichani), gazeti hili lina full Data.

Hassani William Moshi ‘TX Junior’ akiwa katika pozi
Tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu muda mfupi baada ya wawili hao kutoka katika Club ya Habour’s iliyopo Kurasini Temeke jijini Dar es Salaam na mrembo huyo kwenda kuripoti katika Kituo cha Polisi Kilwa…

WANAPIGA MZIGO... BILA MBWEMBWE

Stori: Erick Evarist
KILA mtu ana staili yake katika kufanya kazi inayomuingizia kipato, wapo wasanii wa filamu wanaofanya kazi zao waziwazi na wengine hupenda kujificha.
Amani linashuka na listi ya wasanii ambao wapo ndani ya gemu kitambo lakini staili yao si ya ‘kuanika’ sana kazi zao.

JACOB STEVEN JB:
Anapiga mzigo chini ya kampuni yake ya Jerusalemu Film Company. Staili yake ya maisha unaweza kusema hayupo vile, asikwambie mtu jamaa anapiga mzigo, anakubalika na aliwahi kushinda tuzo za Ziff katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume mwaka 2011.…

PASTOR MYAMBA ASHUSHA MAOMBI BARABARANI

Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’
Stori: Gladness Mallya
MSANII ambaye mara nyingi huigiza kama mchungaji, Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amenaswa akimfanyia maombi msanii mwenzake, Koletha Raymond ‘Coletha’ barabarani.
Tukio hilo la aina yake lilipigwa chabo juzikati na paparazi wetu maeneo ya Tabata jijini Dar, ambapo Pastor Myamba alionekana
bize kumuombea Coletha ambaye aliumwa kichwa ghafla.
“Shindwa kwa jina la Yesu, pepo toka kwa jina la Yesu,” alisikika Pastor Myamba na baada ya muda Coletha alirejea katika hali ya kawaida.

No comments:

Post a Comment