Stori: Hamida HassanMwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata amekuwa akitumiwa na watu wasiojulikana kuwatepeli watu kupitia mtandao wa Facebook kwa akaunti yenye jina la Flaviana Matata’s huku ikidaiwa kuwa wengi wameshalizwa.
Taarifa
ya Kampuni ya Compass Communications inayosimamia kazi za modo huyo
inaeleza kuwa, watu hao wasiojulikana wamefungua akaunti kwenye mtandao
wa Facebook na kuwarubuni watu kuwa, ‘Flaviana’ huyo anawatafutia kazi
wasichana nje ya nchi kwa gharana ya shilingi hadi 200,000.“Tunawatahadharisha watu kuwa Flaviana hatafutii wasichana kazi ya uanamitindo, wanaotumia akaunti ya Flaviana Matata’s ni genge la wahalifu, akauti sahihi ya Flaviana ni Flaviana Lavvy Matata,” ilieleza taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment