-KISA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA
Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
ILI
kuhakikisha harudi tena kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, jeshi la
polisi nchini, limemweka kati mwanamuziki Rehema Yusuf Chalamila ‘Ray
C’.
Kamanda wa jeshi la polisi, kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya
nchini, Godfrey Nzowa, amesema kuwa Ray C kila anapotembea anakuwa
katikati ya askari wanaofuatilia nyendo zake.
“Kila anapokwenda,
askari wamemzunguka. Tangu alipopata nafuu, tumekuwa tukihakikisha
havutiwi na makundi mabaya, vilevile tunataka kuona kweli
amejirekebisha,” alisema Nzowa na kuongeza:
“Ray C mwenyewe haoni
lakini kila anapotoka, askari wanamuweka katikati. Kwa kifupi kipindi
hiki tumemuweka katikati yetu, kwani hata anapokuwa nyumbani,
tunachunguza nani anaingia na anapeleka nini.”
Nzowa aliongeza kuwa
kitengo chake kimeamua kumuweka kati Ray C kwa sababu mbili, moja ikiwa
kubaini na kuwanasa wauzaji wanaomharibu mwanamuziki huyo, pili ni
kufuatilia kama msaada uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete umefanya kazi
yake ipasavyo.
“Mheshimiwa (JK) alitoa msaada wa matibabu kwa Ray C
kwa nia njema, vilevile dada huyo aliapa mbele yake kama hatarudia tena.
Sasa ni lazima kufuatilia na kudhibiti asije kuingia kwenye vishawishi,
akakiuka kiapo na matokeo yake alichokifanya mheshimiwa kikaonekana
hakina maana,” alisema Nzowa.
Kwa upande mwingine, Nzowa alisema,
hali ya Ray C inaendelea kuimarika na akaongeza: “Akili yake imetulia,
anaweza hata kutunga nyimbo tofauti na alivyokuwa. Watu ambao
anafungamana nao kwa sasa ni wazuri, siyo magenge ya wauzaji na
watumiaji wa madawa ya kulevya.”
Ray C, alisharipotiwa kuwa na hali mbaya baada ya kutopea kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya.
Hata hivyo, JK aliamua kujitolea kunusuru maisha ya mwanamuziki huyo kwa kugharamia matibabu yake mpaka apone.
Takriban
miezi mitatu iliyopita, Ray C alitinga ikulu na kumshukuru JK kwa
msaada aliompa, vilevile akawaambia Watanzania kwamba sasa anajisikia
amepona na anaweza kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment