NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Monday, February 25, 2013

MASTAA WA KIKE BONGO; KUTAFUTA USTAA, FEDHA KUTAWADHALILISHA SANA TU!

UPENDO ndiyo dini yangu! Ndiyo maana natumia safu hii kuwarekebisha mastaa wetu ili nitii matakwa ya dini yangu yaani kuwapenda! Hakuna ubishi kuwa umaarufu ni gharama. Ni ghali. Wakati mwingine husababisha kubadili maisha halisi ili kufikia lengo. Ikiwezekana kuondoa utu kwa kujitoa fahamu na kufanya mambo ya kujidhalilisha. Ndivyo ilivyo kwa wasanii wetu. Imewabidi kuishi maisha ya kuigiza ili kujitwalia umaarufu.
Aunt Ezekiel.
Ili kupata umaarufu ni lazima uwe na fedha. Itakubidi ujue sehemu za kwenda kubadilisha mawazo na kustarehe na mastaa wenzako. Siyo sehemu za bei rahisi. Mara nyingi kama staa akijishusha sana, ni kwenye migahawa kama ile ya pale Mlimani City, Dar.
Hawali vyakula vya ovyo. Ni baga na ‘take away’ za gharama. Siyo chipsi vumbi. Hawapandi usafiri wa jumuiya (public transport). Unachezea ustaa wewe?
Ili kukidhi matakwa tajwa hapo juu uitwe staa inawalazimu kutafuta fedha kwa njia yoyote ile ili kugharamia ustaa. Hilo ndilo lililowaponza mastaa wa kike Bongo. Kwa kuwa hawana vipato na wanahitaji maisha ya kujiachia kwenye kumbi za starehe usiku na kulala mchana kutwa, imewabidi kutumia miili yao. Ni kwa kujiuza na kuuzwa kwa wanaume kutoa huduma ya ngono ili kujipatia fedha za kushikilia ustaa. Ama kweli kusaka umaarufu kumewafanya dada zetu kuwa watumwa wa ngono.
Ipo mifano lukuki kwa mastaa walioamua kuwaacha wanaume waliokuwa nao kabla hawajapata umaarufu na kukimbilia kuolewa na watu wenye fedha.
Wolper.
Hata hivyo, kwa kuwa walifuata fedha na siyo mapenzi kwa wanaume hao, walipoishiwa na mapenzi yaliisha. Ndoa ziliota mbawa.
Wapo mastaa wa kike walioshindwa kudumu kwenye ndoa kwa kuwa wanaume waliowaoa waliishiwa na pesa.
Iko wapi ndoa ya kifahari ya Irene Uwoya? Kuna madai kuwa baada ya mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kuishiwa fedha, ndipo dada yetu akazingua.
Unakumbuka ndoa ya kifahari ya Jacqueline Patrick na Abdullatif Fundikira? Ilielezwa kuwa baada ya jamaa huyo kutupwa selo katika Gereza la Keko, Dar kwa kisanga cha mihadarati, Jack alichukua hamsini zake, akijua kabisa kwamba mkwanja umeota mbawa. Hakuwahi kwenda kumuona selo kudhihirisha kuwa hakuwa na mapenzi ya dhati na mumewe huyo bali alifuata mkwanja.
Unakumbuka penzi la Jacqueline Wolper na Abdallah Mtoro ‘Dallas’? Inasadikiwa kuwa baada ya fedha za mshikaji huyo aliyekuwa amemnunulia Wolper gari aina ya BMW X6 kurudi kwao ndipo sistaduu huyo akakata mguu na kusitisha uchumba wao.
Unajua anayempa Wema jeuri ya kubadili magari kama nguo, kutamba kununua nyumba ya mamilioni na kufungua ofisi ya kifahari? Inaelezwa kuwa ni mume wa mtu anayetajwa kwa jina la Clement au CK, kigogo katika idara nyeti nchini.
Aunt Ezekiel ameolewa na Sunday Demonte, jamaa mwenye mkwanja mbuzi ambaye hata hivyo hawaishi wote. Aunt yupo Bongo akisubiri kutumiwa fedha ya matumizi na bwana huyo aliyeko Dubai.
Hivi karibuni Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ alinaswa na mapaparazi wa Global akiuzwa kwa dola 500 akafanye ngono na mwanaume aliyejifanya Mtanzania aishie Marekani. Ni aibu lakini atafanyaje ili kukidhi vigezo vya ustaa? Lazima awe na fedha kwa njia yoyote. Ipi? Kukubali kuuzwa kingono.
Nimetoa mifano michache mno lakini ni mingi. Ukweli ni kwamba hali ni mbaya. Wasipobadilika, wataendelea kudhalilika sana tu kabla ya madhara mengine ikiwemo kuambukizwa magonjwa hatarishi hasa Ukimwi. For the love of game!

No comments:

Post a Comment