NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Wednesday, January 23, 2013

BIFU LA SHILOLE NA FLORA MVUNGI LIMEZIDI KUCHUKUA SURA MPYA


 BIFU kali la wasanii wawili wa filamu nchini Tanzania  Flora Mvungi na Shilole limezidi kuchukua sura mpya baada ya Flora kupania kuwatafuta watu wote wanaoshirikiana na Shilole kwa kuongea maneno machafu juu yake

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Flora Mvungi alisema chanzo cha ugomvi huo hakielewi ila anashangazwa na maneno yanayorushwa kila siku na msanii huyo mwenzake kupitia baadhi ya vyombo vya habari huku akiamini kuwa hayupo pekee yake katika mchakato huo

Alisema kuwa kutokana na Shilole kutokuwa na uwezo wa kutumia mitandano ya kijamii na maneno machafu hayo yanatumwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii hivyo kwa vyovyote nyuma yake kuna watu wanaomsaidia kufanya hivyo

Kutokana na hilo Flora alisema kuwa amejipanga kuwatafuta watu wote wanaoshirikiana na Shilole kuendeleza ugomvi huo ili waeleze chanzo na sababu ya ugomvi huo wa pande hizo

Alisema anashangazwa na tabia ya msanii huyo kuongea vibaya akiwa na watu wengine na anapokuwa na yeye anaongea kistarabu kama vile hakuna kitu chochote kati yao kinachoendelea

Mvungi aliendelea kuelezea kuwa baada ya kugundua hilo alitafuta njia ya kumaliza tofauti zao lakini ilishindikana kwa kuwa Shilole hakuwa tayari kupokea simu wala kufanya mazungumzo pamoja naye

"Nahisi labda wivu kwani mara ya kwanza tulikuwa marafiki wazuri lakini baada ya mimi kuwa na mahusiano na H.Baba sasa nimekuwa karibu sana na mchumba wangu inawezekana ikawa ni sababu ya kunionea wivu" alisema Flora Mvungi

Kwa upande wake msanii maarufu Shilole alipoulizwa kuhusu madai haya, yeye alifafanua kuwa anashangazwa na kitendo cha msanii mwenzake kuongea hovyo huku akiwa hana uwakika na anachokizungumza

Alisema kwa upande wake yeye hawezi kuzungumzia chochote kile kwani hana tatizo la mtu ila Frola atakuwa anajua tatizo liko wapi ndio maana anakuwa na uwezo wa kuyaongelea hayo

"Mengi nimeyasikia akizungumza nimeamua kukaa kimya na kutumia busara zaidi kwani niko makini na kazi zangu na sitaki kuchafua jina langu amabalo teyari limeshakuwa na sura mpya kwa jamii" alisema Shilole

Akiongelea kuhusu kutafuta njia ya kusuruhisha ugomvi huo alisema hana utaratibu wowote ule wa kumtafuta msanii mwenzake ili waweze kuzungumza tofauti zao kwani kwa upande wake hana nafasi ya kuzungumza lolote

"Unajua kuna baadhi ya watu wamepotea kwenye fani sasa wanatafuta njia ya kurudi na kusikika kwa njia ya kuzusha mabifu kitu ambacho kwangu ni tofauti sana mimi sitoruhusu hiyo hali kwangu ndio maana nimeamua kukaa kimya " alisema Shilole

No comments:

Post a Comment