
KUTOKANA na ndoa hiyo kuwa ya aina yake, hivi karibuni waandishi wetu walimuweka kati Bob Junior na kumbana kwa maswali ya “why, kwanini, ikawaje” aoe kimyakimya wakati yeye ndiye ‘prezidaa’ wa masharobaro?

Bob Junior akafunguka: “Nilifunga ndoa Desemba mwaka jana. Nililazimika kuoa kimyakimya kutokana na masharti ya wazazi wa pande zote mbili kwamba ndoa isifungwe kwa mbwembwe.”
Alisema, hata idadi ya wahudhuriaji katika ndoa hiyo ilidhibitiwa, hivyo kuruhusu ndugu na marafiki wachache kushuhudia tukio hilo.…

WOLPER AFUNGUKIA UHUSIANO WAKE NA SAJUKI

SIKU chache baada ya kifo cha mwigizaji Juma Kilowoko, mwigizaji Jacqueline Wolper amefungukia uhusiano wake na marehemu hadi kufikia hatua ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu.
Akizungumza na Funguka na Risasi kwenye msiba wa msanii huyo pande za Tabata Bima jijini Dar, Wolper alisema Sajuki alimpenda kama kaka yake wa damu ndiyo maana alikuwa tayari kumsaidia kwa hali na mali.


JACK MAISHA PLUS, RUBI WAFANYA MAZOEZI KUONDOA ‘VITAMBI’

MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dastan ‘Jack Maisha Plus’ na shosti wake ambaye ni bosi wa Kundi la Nderemo Arts Group, Khadija Kasongo ‘Rubi’ wameanza kufanya mazoezi ya viungo kwa lengo la kuondoa ‘vitambi’.
Wasanii hao wameamua kuingia kwenye ‘tizi’ baada ya kuona vitambi vinakuwa tishio kwao, jambo ambalo limekuwa likiwakosesha raha kwani wanahisi hawana mwonekano mzuri.
“Tunafanya mazoezi asubuhi na…

NDIKUMANA WA UWOYA ANAUMWA

MSAKATA kabumbu mkali nchini Rwanda ambaye pia ni mume wa diva wafi lamu za Kibongo, Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Katauti ’ ni mgonjwa kiasicha kushindwa kuendelea kuichezea timu yake ya Rayon Sports ya Rwanda.
Akiwasiliana na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya mtandao wa kijamii wa ‘Facebook’,Ndikumana alisema kuwa kwahivi sasa hali yake siyo nzuri kiafyana ndiyo maana ameshindwa kujiunga na mazoezi ya timu yake hiyo.
“Kwa hivi sasa bado naumwa,hivyo sija ichezea timu yangu mchezo wowote mpaka afya yangu itakapo…

HILI NI DARASA HURU, KUCHUJA PENZI HALISI NA MAZOEA - 5

Inawezekana kweli ameyafanya maisha yako kuwa na furaha lakini hiyo furaha anaidumisha vipi? Isije ikawa anakufurahisha pale tu anapokuwa na shida zake, pindi unapomtatulia huyo anakwenda zake, akirudi tena ujue ana shida.


KUMBE WENYE BAA WENGI WANAZUIA JUA BADALA YA MVUA!

Wateja wengi wakiona baa ipo hivyo, wanamiminika kuliko hata wanavyokwenda kwenye nyumba za ibada.
Lakini tatizo linakuja kipindi mvua inaponyesha! Baa nyingi huwa zinavuja kiasi cha kuwafanya wateja wakimbilie sehemu nyingine kujisitiri wasilowane.
Hii inaonesha kwamba, wamiliki wa baa hizo wanatumia akili zao kupambana na jua lisiwapate wateja wao na si mvua. Wamiliki hao waliangalie hilo kuanzia sasa kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa itaendelea kunyesha nchini mpaka mwezi Machi mwaka huu.…
No comments:
Post a Comment