NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Sunday, January 20, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATATU 21/1/2013

ISABELA, KALAMA WANANGWA MTANDAONI

Luten Kalama na mpenzi wake Isabela Mpanda.
Na Gladness Mallya

WAPENZI mastaa, Luten Kalama na Isabela Mpanda wameambulia matusi mfululizo baada ya kuweka picha mtandaoni inayowaonesha wakiwa wanadendeka.

Ishu hiyo imetokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mlimwende Isabela kuweka picha hiyo katika akaunti yake ya mtandao wa Facebook ambapo ndani ya muda mfupi alipokea matusi makali na kulazimika kuindoa haraka.

“Waswahili bwana wasione watu wanapendana ishakuwa nongwa, ngoja niitoe. Isiwe tabu,” aliandika Isabela…

AMANDA: MISOSI ANADEKA

Na Gladness Mallya
STAA wa filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa kipenzi chake, Emmannuel Rushau ‘Bwana Misosi’ anapenda kudeka pindi wanapokuwa viwanja.
Akipiga stori na paparazi wetu katika Viwanja vya Leaders Club hivi karibuni, Amanda aliweka plain kuwa ‘boifrendi’ wake huyo amekuwa na tabia hiyo hali ambayo inaleta maswali mengi kwa wasiolipenda penzi lao.
“Jamani Baby wangu naye anadeka... hebu tazama sasa hivi alivyonilalia, majungu yataanza sasa hivi. Lakini nilikuwa nikiomba faraja, sasa nimeipata nashukuru,” alisema Amanda.

BABY MADAHA: SEGEREA INAMUITA SHILOLE

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Na Gladness Mallya

KUTOKANA na bifu linalofukuta kama moto wa kifuu kati ya waigizaji, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’, staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameibuka na kumchana Shilole kuwa analitamani Gereza la Segerea.

Akichonga na paparazi wetu, Baby Madaha ‘aliyelinunua’ sakata hilo, alimtaka Shilole kuacha kumfuatafuata shosti wake (Flora) kwani yeye hana lolote zaidi ya kuropoka maneno machafu.

“Eti Shilole anatangaza kuwa atanipiga mimi hebu ajaribu kama yeye mwanamke kweli, mimi haniwezi kamwe. Kwanza hajielewi hata thamani yake, kutwa kutembea na watoto wadogo halafu anajiona staa,” alisema Baby…

SAJUKI, WASTARA KATIKA MAANA HALISI YA MAPENZI, TUJIFUNZE-3

MUNGU ni sababu ya kila kitu. Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ ameshatangulia mbele ya haki. Jambo zuri kwetu sisi ni kujifunza kwa yale aliyoyaacha kama mfano wa kuigwa. Yeye na mkewe, Wastara Juma Issa, wameonesha kitu kikubwa sana katika uhusiano wa kimapenzi.

Wanaume waamue kupenda na kukubali mitihani ya namna yoyote itakayowakuta wapenzi wao. Wafanye kama alivyoweza Sajuki pale mwenzi wake Wastara alipopata ajali, akakatika mguu. Inawezekana tu kama unakuwa na moyo wa kweli.

Wanawake washike njia ya Wastara. Maradhi au matatizo ya aina yoyote watakayoyapata wapenzi wao, kwao iwe ni changamoto ya kulazimisha kuivuka. Kuna heshima na baraka nyingi katika kufanya kama alivyotenda Wastara kwa Sajuki.

Vilevile, ieleweke kuwa kuna laana katika kumkimbia mwenzi wako pale anapopatwa na matatizo.…

KWENYE BONGO FLEVA SAWA LAKINI MSITUONESHE ‘VITUMBUA’

TAKRIBAN miaka 20 iliyopita, baadhi ya mastaa wa Nollywood, Nigeria walianza kwa kuigiza. Waliigiza kwa kujituma sana ili kujitengenezea jina kwa ajili ya soko la filamu zao ndani na nje ya nchi yao.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Katika jitihada hizo, baadaye wakaona wajichanganye kwenye muziki. Haikuwa kazi ndogo. Mmoja wao ni Omotola Jalade Ekeinde. Nilizungumza naye alipotua nchini mwaka jana.

Aliniambia kuwa kuna wakati mwingine walifanya kazi bila malipo. Lengo lilikuwa ni moja tu, kujitangaza kwa ajili ya baadaye. Waliamini kitu kikubwa kinakuja. Kweli wamefanikiwa. Wamejitengenezea himaya kule…

POLISI MBEYA NUSURA WACHOMWE MOTO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya

MKAZI mmoja wa Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Joseph Mwaenga (32) ambaye ni mwendesha pikipiki amenusurika kujilipua na kulipua kituo cha polisi mjini hapa akipinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na askari hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman amewaeleza waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa tukio hilo limetokea saa 5 usiku katika eneo la kituo hicho.

Alisema kuwa kijana huyo ambaye ni mwendesha bodaboda alifikishwa  kituoni hapo baada ya kufanya vurugu katika kijiwe cha maegesho ya pikipiki na baada ya hapo alipokonywa pikipiki yake  na wananchi na kuifikisha…
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MKAZI mmoja wa Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Joseph Mwaenga (32) ambaye ni mwendesha pikipiki amenusurika kujilipua na kulipua kituo cha polisi mjini hapa akipinga vitendo vya uonevu vinavyofanywa na askari hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman amewaeleza waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa tukio hilo limetokea saa 5 usiku katika eneo la kituo hicho.
Alisema kuwa kijana huyo ambaye ni mwendesha bodaboda alifikishwa  kituoni hapo baada ya kufanya vurugu katika kijiwe cha maegesho ya pikipiki na baada ya hapo alipokonywa pikipiki yake  na wananchi na kuifikisha polisi.
Hata hivyo, baada ya kufikishwa kituoni hapo akiwa nje ya kituo alijimwagia mwilini petroli aliyokuwa nayo ndani ya dumu na kumwagia kituo cha polisi  kisha kutoa kiberiti na kutaka kujilipua yeye na kituo hicho kabla ya kudhibitiwa na askari wa zamu.
Alisema kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza kwa binadamu wala mali juu ya tukio hilo na mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia  sasa.

TOTTENHAM, MANCHESTER UNITED HAKUNA MBABE

Mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie (20) akiifungia timu yake bao la kuongoza kwa kichwa likiwa ni bao lake la 22 msimu huu katika dakika ya 25 ya mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa White Hart Lane jijini London.
Clint Dempsey wa Tottenham (kulia) akisawazisha bao katika dakika ya 93 na…
Mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie (20) akiifungia timu yake bao la kuongoza kwa kichwa likiwa ni bao lake la 22 msimu huu katika dakika ya 25 ya mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa White Hart Lane jijini London.
Clint Dempsey wa Tottenham (kulia) akisawazisha bao katika dakika ya 93 na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka mwisho wa mchezo.



No comments:

Post a Comment