NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Wednesday, January 16, 2013

MBATIA ANUSURIKA KUUAWA MTWARA


MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amekatisha ziara yake mkoani Mtwara baada ya jana kunusurika kuuawa na baadhi ya wananchi waliudhuria mkutano wake wa adhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa mjini hapa kwa madai hawakuridhishwa na hotuba yake.
Mbatia na wabunge wake Moses Machali (Kasulu mjini) na Agripina Buyogela (Kasulu vijijini) waliokolewa na polisi baada ya kujifungia katika ofisi za chama hicho wilaya ya Mtwara Mjini kwa zaidi ya saa moja na nusu kuanzia saa 12 kasoro ya jioni hadi saa 1: 17 polisi walipowasili eneo hilo.
Wananchi walizingira ofisi hiyo huku wakiimba nyimbo za kumshtumu Mbatia kuwa ni Mamluki aliyetumwa na serikali kulainisha msimamo wa wananchi wa mkoa huo kuhusu gesi inayovunwa kijiji cha Msimbati kutopelekwa Dar es Salaam.
Kadri jua lilivyokuwa linazama na giza kutanda ndivyo hali ya usalama wa viongozi hao ilivyozidi kuwa tete, wananchi walianza kutupia mawe ofisi hiyo na wengine kujaribu kuvunja mlango kwa kurushia vitu vinavyosadikiwa ni mabomu ya kuulia samaki baharini…….
  14 MBATIA ANUSURIKA KUUAWA MTWARA

No comments:

Post a Comment