NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Wednesday, January 16, 2013

Mji wa Konna ungali chini ya waasi Mali


 16 Januari, 2013 - Saa 07:37 
Wanajeshi wa Ufaransa wanasema waasi wangali wanaudhibiti mji wa Konna
Maafisa katika jeshi la Ufaransa, wamekanusha madai yaliyotolewa awali na jeshi la Mali, kuwa wameweza kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa umetekwa na waasi.
Ufaransa, ilianza harakati zake za kijeshi kusaidia jeshi la Mali dhidi ya waasi Ijumaa iliyopita baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuuteka mji wa Konna na kuanza kuukaribia mji mkuu.
Mji mwingine wa Kati ,Diabaly, ulitekwa na waasi Jumatatu iliyopita.
Wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wa Mali, wameanza kuelekea katika mji huo kuanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya waasi.
Mwezi Machi mwaka jana wapiganaji wa kiisilamu wakishirikiana na waasi wa Tauareg, waliteka Kaskazini mwa Mali.
Hivi karibuni wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, walidhibiti eneo hilo na kuanza kuweka sheria kali za kiisilamu.
Pindi mpango wa serikali wa kuutwaa mji huo , waasi nao wakaanza kuelekea Kusini mwa nchi.
Rais Francois Hollande
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alisema kuwa Ufaransa ina lengo moja tu, kuhakikisha inaondoka Mali, baada ya nchi hiyo kuwa salama na kuhakikisha kuwa hakuna tisho lengine la kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
Hatua ya wanajeshi kuteka mji muhimu wa Konna wiki jana , ndiyo ilichochea Ufaransa kuchukua hatua za kijeshi kusaidia Mali.
Ndege za Ufaransa, zilianza kufanya mashambuliziya angani dhidi ya wapiganaji hao siku iliyofuata hadi Jumamosi.
Maafisa walisema kuwa jeshi la Mali lilisema limeweza kudhibiti mji wa Konna na kwamba wapiganaji
100 waliuawa.
Lakini waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, aliambia waandishi wa habari mjini Paris kuwa mji huo bado uko mikononi mwa waasi.
Ndege za kijeshi za mali ziliweza kuzuia waasi waliokuwa wameingia eneo lililo katikati mwa miji ya Douentza na Gao.
Duru hata hivyo zinaarifu kuwa jeshi la Mali halina uwezo mkubwa wa kudhibiti waasi kivyao


No comments:

Post a Comment