NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Thursday, January 10, 2013

Milion 16 Alizo toa Wolper kwa Ajili ya Matibabu kwa Sajuki zaleta Maneno


KAMA unakumbuka msanii Jackline Wolper alimpatia sh mil 16 Sajuki kwa ajili ya matibabu nchini India, sasa yameanza kuibuka mengine ambapo inadaiwa kuwa kiasi hicho cha fedha alichukua kwa mtu na mwenye nazo ameshindwa kuvumilia ameamua kuanza kumdai ili azirudishe tofauti na makubaliano yalivyokuwa.

Inadaiwa kuwa habari hizo zilianza kuzuka tangu siku ambayo Sajuki amefariki, huku mwenye fedha hizo akidai kuwa alitoa fedha hizo kwa makubaliano kwamba atarudishiwa mapema lakini hadi muda waliopangwa umepita haoni dalili zozote za kupewa fedha zake.

Chanzo kimoja cha kuaminika kilizungumza na mwandishi wa DarTalk na kutoa story ilivyo, ambapo kilidai kuwa ishu hiyo imeanza kujitokeza upya siku ya msiba na wenyewe walitaka kulipana kimya kimya lakini baada ya maneno kuwa makubwa wamepanga kulipana muda wowote sasa.

Hata hivyo chanzo hicho kilisema kuwa Wolper hakutakiwa kutoa kiasi chote cha pesa kwa Sajuki lakini alifanya hivyo ili kuonekana mbele za watu kuwa ndiye aliyefanya mambo makubwa wakati hamna kitu.

“Msibani maneno yalikuwa yanazungumzwa sana tena chini kwa chini mwenyewe Wolper kainamisha kichwa chini kwa aibu asa sijui atazilipa maana huyo mwenye nazo ni mbongo wa kawaida lakini si mtu wa njaa kama sisi bongo movie,” alisema

No comments:

Post a Comment