NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

BRAZIL BADO INASAFARI NDEFU KUFIKIA MAFANIKIO - NEYMAR.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amedai kuwa nchi yake ina safari ndefu kama wanahitaji kulibakisha Kombe la Dunia nchini kwao mwaka ujao. Katika mahojiano na vyombo vya habari mara ya timu yake kubanguliwa mabao 2-1 na Uingereza katika Uwanja wa Wembley Neymar amesema timu yake inatakiwa iboreshe mchezo wake ili uwe wa kiushindani zaidi. Nyota huyo ambaye anafanishwa na nguli wa zamani wa soka Pele alidai kuwa wakiwa kama wenyeji wa michuano hiyo watakuwa katika shinikizo zaidi lakini labda mashabiki wao wanaweza kuwasaidia kulinyakuwa kombe hilo. Brazil kwasasa imeporomoka katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mpaka kufikia katika nafasi ya 18. Neymar ambaye mkataba wake na klabu ya Santos unaishia mwaka 2014 pia alidai kuwa ndoto zake wakati akiwa mdogo ni kwenda kucheza soka barani Ulaya na kuchagua nchi za Ujerumani na Hispania kama sehemu ambapo anaweza kwenda wakati mkataba wake utakapomalizika.

No comments:

Post a Comment