NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

MISS TZ AFANYA KUFURU USA

PICHA za tukio la ‘bethidei’ ya mwanamitindo maarufu wa Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2001, Millen Magese ‘Happiness’ iliyofanyika hivi karibuni huko New York, Marekani, ilikuwa ni kufuru tupu.
Kupitia mtandao wa Instagram, modo huyo ambaye makazi yake ni Afrika Kusini ‘Sauzi’, aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kumpa sapoti ya kutosha kwenye tukio hilo ambalo lilipewa jina la Birthday to Remember With Super Modal Millen and Friend.
“Nawashukuru sana jamani, bethidei yangu ilikuwa baab’kubwa hivyo asanteni wote,” aliandika Millen mtandaoni.
Katika pati hiyo, watu walijiachia kwa misosi kiwango, vinywaji vya bei mbaya na kuserebuka muziki huku wakishindwa kuamini kama ni mrembo huyo aliyeamua kuangusha sherehe hiyo.


No comments:

Post a Comment