NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

Flora Mvungi Stori: George Kayala wiki iliyopita tuliwasikia mastaa wa muziki na filamu za Kibongo, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wakifunguka juu ya bifu lao zito linaloonekana kukosa ukomo. Nilizungumza na wasanii juu ya kuwakutanisha wiki hii ili tufunge ukurasa wa bifu lao lakini majibu yalikuwa ni tofauti kabisa na matarajio. Nini kilichotokea? Fuatana nami sasa… Shilole Funguka: Shilole habari za tangu wiki jana? Shilole: Nzuri, naona umeibuka tena. Funguka: Kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba wiki hii ni lazima niwakutanishe wewe na Flora. Kabla ya kuendelea, hebu wakumbushe wasomaji wangu wiki iliyopita ulisemaje nilipotaka kukukutanisha na Flora? Shilole: Nilisema siwezi kukutana na Flora kwani nina mambo mengi ya kufanya na kinachonishangaza ni kwamba yeye anachonga kwenye vyombo vya habari mambo yake ili ionekane mimi ndiye ninamchafua. Siwezi kupoteza muda wangu kuzungumzia suala la msanii huyo kwani anasaka umaarufu kwa kutumia jina langu. Funguka: Kwani wewe na Flora aliyetangulia kuwa na jina kubwa katika sanaa ni nani? Shilole: Ni yeye lakini mimi nimekuja nyuma yake na nyota yangu ya sanaa imeng’aa na kumpita, ndiyo maana sasa anahaha kusaka kurejesha jina lake kwa kutumia mgongo wangu. Mimi niko juu yake kwani Mungu amefanikisha kufika hapa nilipo. Funguka: Mbona siwaelewi, Flora anasema wewe ndiye ulianzisha ugomvi kwa kuanika kwenye vyombo vya habari kwamba amefulia kisanaa baada ya kuhamishia penzi lako kwa H. Baba (Hamis Ramadhan). Inavyoonekana ninyi wote mnachezea akili za Watanzania kwa kujionesha mna bifu kumbe mnakuza majina yenu kiaina? Shilole: Siyo kweli. Mimi nina uwezo wa kisanaa hivyo siwezi kutegemea kutengeneza bifu na msanii mwenzangu kwani kazi zangu zinaniwezesha kuniweka katika chati nzuri ya muziki wa kizazi kipya na filamu. Funguka: Sawa, vipi kuhusu suala la kukutana na Flora ili mmalize tofauti zenu? Shilole: Siko tayari kukutana na mwanamke huyo, nina mambo mengi ya kufanya na sasa ninavyoongea na wewe naelekea studio kurekodi ngoma yangu nyingine. Siwezi kupoteza muda kwa kukaa na dada anayetaka kusafisha nyota yake kupitia mgongo wangu. Funguka: Dah! Nikuache uendelee na majukumu yako ngoja nigeukie kwa Flora, nione kama naye anasema nini juu ya kukutana nawe ili tufunge mjadala huu. Shilole: Sawa. Funguka: (Baada ya muda) Napiga namba yake siipati sijui ana tatizo gani? Shilole: Sijui, jaribu kumtafuta shosti wake Baby Madaha anaweza kukwambia kitu. Funguka: Kwani naye anahusika na bifu lenu? Shilole: Ndiyo, naye si alijiingiza mpaka amediriki kusema mimi natumia madawa ya kulevya. Funguka: Dah! Ngoja nimtafute. Shilole: Poa kaka. Funguka: Baby Madaha habari yako, niambie, nasikia na wewe umenunua ugomvi wa Shilole na Flora kwa nini umefanya hivyo? Baby Madaha: Ni kweli, Shilole ni mtoto kwetu, ikumbukwe kuwa Flora ni wifi yangu kwa H. Baba hivyo siko tayari kuona anaonewa bila sababu za msingi na lengo lake ni kutaka kuharibu uchumba wao.

Flora Mvungi
Stori: George Kayala
wiki iliyopita tuliwasikia mastaa wa muziki na filamu za Kibongo, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wakifunguka juu ya bifu lao zito linaloonekana kukosa ukomo.
Nilizungumza na wasanii juu ya kuwakutanisha wiki hii ili tufunge ukurasa wa bifu lao lakini majibu yalikuwa ni tofauti kabisa na matarajio. Nini kilichotokea? Fuatana nami sasa…
Shilole
Funguka: Shilole habari za tangu wiki jana?
Shilole: Nzuri, naona umeibuka tena.
Funguka: Kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba wiki hii ni lazima niwakutanishe wewe na Flora. Kabla ya kuendelea, hebu wakumbushe wasomaji wangu wiki iliyopita ulisemaje nilipotaka kukukutanisha na Flora?
Shilole: Nilisema siwezi kukutana na Flora kwani nina mambo mengi ya kufanya na kinachonishangaza ni kwamba yeye anachonga kwenye vyombo vya habari mambo yake ili ionekane mimi ndiye ninamchafua. Siwezi kupoteza muda wangu kuzungumzia suala la msanii huyo kwani anasaka umaarufu kwa kutumia jina langu.
Funguka: Kwani wewe na Flora aliyetangulia kuwa na jina kubwa katika sanaa ni nani?
Shilole: Ni yeye lakini mimi nimekuja nyuma yake na nyota yangu ya sanaa imeng’aa na kumpita, ndiyo maana sasa anahaha kusaka kurejesha jina lake kwa kutumia mgongo wangu. Mimi niko juu yake kwani Mungu amefanikisha kufika hapa nilipo.
Funguka: Mbona siwaelewi, Flora anasema wewe ndiye ulianzisha ugomvi kwa kuanika kwenye vyombo vya habari kwamba amefulia kisanaa baada ya kuhamishia penzi lako kwa H. Baba (Hamis Ramadhan). Inavyoonekana ninyi wote mnachezea akili za Watanzania kwa kujionesha mna bifu kumbe mnakuza majina yenu kiaina?
Shilole: Siyo kweli. Mimi nina uwezo wa kisanaa hivyo siwezi kutegemea kutengeneza bifu na msanii mwenzangu kwani kazi zangu zinaniwezesha kuniweka katika chati nzuri ya muziki wa kizazi kipya na filamu.
Funguka: Sawa, vipi kuhusu suala la kukutana na Flora ili mmalize tofauti zenu?
Shilole: Siko tayari kukutana na mwanamke huyo, nina mambo mengi ya kufanya na sasa ninavyoongea na wewe naelekea studio kurekodi ngoma yangu nyingine. Siwezi kupoteza muda kwa kukaa na dada anayetaka kusafisha nyota yake kupitia mgongo wangu.
Funguka: Dah! Nikuache uendelee na majukumu yako ngoja nigeukie kwa Flora, nione kama naye anasema nini juu ya kukutana nawe ili tufunge mjadala huu.
Shilole: Sawa.
Funguka: (Baada ya muda) Napiga namba yake siipati sijui ana tatizo gani?
Shilole: Sijui, jaribu kumtafuta shosti wake Baby Madaha anaweza kukwambia kitu.
Funguka: Kwani naye anahusika na bifu lenu?
Shilole: Ndiyo, naye si alijiingiza mpaka amediriki kusema mimi natumia madawa ya kulevya.
Funguka: Dah! Ngoja nimtafute.
Shilole: Poa kaka.
Funguka: Baby Madaha habari yako, niambie, nasikia na wewe umenunua ugomvi wa Shilole na Flora kwa nini umefanya hivyo?
Baby Madaha: Ni kweli, Shilole ni mtoto kwetu, ikumbukwe  kuwa Flora ni wifi yangu kwa H. Baba hivyo siko tayari kuona anaonewa bila sababu za msingi na lengo lake ni kutaka kuharibu uchumba wao.

No comments:

Post a Comment