Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
IMEBAINIKA
kuwa lile gari la aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven
Kanumba, aina ya Toyota Lexus limekabidhiwa kwa mwigizaji, Mahsein
Awadhi ‘Dk. Cheni’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mama wa marehemu,
Flora Mtegoa alifikia uamuzi wa kumkabidhi Dk. Cheni gari hilo baada ya
kushindwa kuligharamia mafuta.
“Lilikuwa linakaa muda mrefu pale
nyumbani kwao Kimara-Temboni (Dar) bila kutumika ndipo bi mkubwa akaona
bora amkabidhi Dk. Cheni ili angalau aliendesheendeshe lisiharibike,”
kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini.
DK. CHENI LIVE TABATA
Wakati mapaparazi wakianza
kazi ya kuchimba data zaidi juu ya gari hilo, Februari 9, walimnasa Dk.
Cheni akiingia na gari hilo kwenye arobaini ya marehemu Juma Kilowoko
‘Sajuki’ iliyofanyika nyumbani kwake Tabata-Bima, jijini Dar.
LIMEPIGWA BEI?
Kwa mujibu wa Dk. Cheni kwa sasa
gari hilo lipo mikononi mwake akilitumia kwa safari za hapa na pale ili
kulifanya lisiharibike vifaa kwa kukaa muda mrefu bila kutumika.
“Wamenipa
nilitumie kwa muda kwani lingeendelea kukaa pale basi lingeendelea kufa
baadhi ya vifaa, wala halijapigwa bei,” alisema Dk. Cheni.
Katika
hatua nyingine, kauli ya mama Kanumba kuhusiana na gari hilo
ilitofautiana na ya mdogo wa marehemu, Seth Bosco ambapo mama huyo
alisema gari hilo halijatoka nyumbani huku mdogo mtu huyo akisema
limetoka.
“Mbona gari lipo hapa nyumbani halijatoka, kwanza limeisha bima na matairi hayana upepo sasa litatokaje?” alihoji mama Kanumba.
Seth alipoulizwa kuhusiana na uwepo wa gari hilo nyumbani, alitiririka:
“Gari limetoka kwa muda hata hivyo ni bovu na linahitaji marekebisho kidogo.”
No comments:
Post a Comment