NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

MAKUNDI YA WANAWAKE NA MITAZAMO YAO KWA WANAUME - 3

Kwa kumalizia uchambuzi wa kundi la kwanza ambalo nilieleza kuwa linaundwa na wanawake wenye umri mdogo ambao hupenda wanaume kutokana na muonekano, vema nitaje bahati mbaya ambazo wanaweza kukutana nazo.Wanawake wa kundi hili huwa na bahati mbaya moja kubwa ambayo ni kusalitiwa na wanaume.
Sababu ni kuwa wanaume hao mara nyingi hutawaliwa na kiburi kwamba wao ni wazuri na wanapendwa, kwa hiyo hukosa msimamo na utulivu wa kweli.
Kwa vile hupenda kulelewa, hutoka na wanawake wengine ambao wataonekana wana fedha zaidi. Kadhalika, hujiona wao ni tabaka maalum sana, kwa hiyo huwa wanataka wanyenyekewe hata kama ni kwa jambo ambalo linawahitaji kunyenyekea.
Wenye tabia ya kupenda wanaume kutokana na muonekano wapo wengi, kwa hiyo unaweza kupenda kesho yake asubuhi mwingine naye akamtaka mwanaume huyohuyo wa kwako, hivyo kuleta ushindani wa kimaslahi kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
Tafsiri ya jumla ni kwamba wanaume ambao humulikwa na wanawake wa kundi hili, aghalabu huwa siyo waaminifu. Kutokana na hali hiyo, wanawake hao mara nyingi husumbuliwa na mateso ya mapenzi, wakilalamikia jinsi wanavyotendwa au wasivyo na bahati ya kupendwa.

KUNDI LA PILI
Kwa kawaida, kundi hili halina tabaka la umri. Wanaounda kundi hili wanaweza kuwa wasichana wadogo au hata wanawake watu wazima. Kipaumbele chao siku zote huwa ni kupata wanaume ambao watawalea, yaani watakaokidhi haja zao.
Wanaweza kuangukia hata kwa wanaume wasiowapenda ilimradi wapate unafuu wa kuishi vizuri. Wao huwa hawana kile kitu kinachoitwa ‘mapenzi ya dhati kutoka moyoni’, isipokuwa hujenga mazoea mpaka huhisi wanapenda au wanapendwa.
Kutokana na ukweli huo kwamba huwa hawazingatii mapenzi ya dhati kutoka moyoni, wanawake wanaounda kundi hili huwa hawachagui umri wa wanaume. Iwe ni kwa vijana wadogo mpaka wazee wenye umri sawa na vikongwe.
Mrembo mwenye umri wa miaka 24, anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mzee mwenye umri wa miaka 70 ambaye kiuhalisia ni babu yake, hilo haliwezi kuwa jambo geni, isipokuwa kilichozingatiwa na mwanamke husika ni unafuu wa kuishi.
Wanawake wa kundi hili, hushawishika kutokana na jinsi wanavyopokelewa na wanaume. Namna ambavyo mwanaume anavyowajibika katika utoaji wa huduma za kimsingi na hata za ziada kwa mwanamke wa kundi hili, humfanya apate alama nyingi za ushindi.
Itaendelea wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment