NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Thursday, February 14, 2013

STAA WA KAKA 'ATEMBEA' NA LINNAH!

Stori: Musa Mateja
KIJANA aliyejipatia umaarufu kwa kumvamia msukuma kambumbu wa Real Madrid, ‘Kaka’, Nagari Kombo amedaiwa kuwa ndiye anayemiliki penzi la Mbongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linnah’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana kwenye viwanja tofauti vya starehe na mara kwa mara wamekuwa wakishea vitu vyao ikiwamo gari la Linnah.
“Mbona siyo siri, Linnah na Nagari ni wapenzi kitambo na siku hizi wanajiachia bila kificho kwa raha zao. Hawamuogopi mtu,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Paparazi wetu alipomtafuta Linnah kuhusiana na ishu hiyo, alipokea simu na alipoulizwa kinachoendelea baina yao alikata simu fasta na kuizima kabisa.

No comments:

Post a Comment