NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Thursday, February 14, 2013

NIGERIA IMEPANDA VIWANGO VYA FIFA, TANZANIA JE? STORI NDIO HII


.
Nigeria imepanda kwa nafasi 22 hadi kufika kwenye nafasi ya 30 kwenye viwango vya FIFA vya dunia ikiwa ni baada ya kufanikiwa kushinda kombe la mataifa ya Afrika 2013 kwa kuifunga Burkina-faso 1-0.
Kabla ya AFCON 2013 Naija ilikua kwenye nafasi ya 52 ambapo licha ya hivyo nchi hiyo imeendelea kuwa nyuma ya Ivory Coast ambayo inabakia kuwa timu namba moja Afrika huku ikishika nafasi ya 12 kidunia, Nigeria ni ya nne kwa Afrika.
Afrika kusini imepanda kwa nafasi 25 zaidi kwenye viwango hivyo vya shirikisho la soka duniani hivyo kufikia nafasi ya 60 kidunia.
Nchi ambazo zimeingia 10 bora Afrika ni pamoja na Algeria, Tunisia, Zambia, Central African Republic, Burkina Faso na South Afrika wakati timu 5 bora za dunia ni Hispania, Ujerumani, Argentina, England na Italia.
Tanzania imeshuka kwa nafasi tatu na sasa hivi inashika nafasi ya 127 pamoja na kwamba iliifunga Cameroon 1-0 hivi karibuni ambapo kama haufahamu, nafasi kubwa kuwahi kushikwa na Tanzania kwenye hivyo viwango ni 65 na hiyo ilikua mwaka 1995.

No comments:

Post a Comment