NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Wednesday, February 13, 2013

LINAH,KASSIM, DULAYO,ZANZIBAR STARS,OMARY TEGO KUIPAMBA VALENTINE DAR LIVE


Mkali wa ngoma za malovee, Kassim Mganga
Linah
Dulayo
Omari tego
LISTI imezidi kuongezeka kwenye shoo maalum ya Siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ itakayochukua nafasi kesho kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo mkali wa ngoma za malovee, Kassim Mganga, Bendi za Zanzibar Stars na Coast Modern Taarab kwa pamoja wameahidi kuongeza nguvu ya burudani.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Burudani wa Dar Live, Luqman Maloto, ukumbi utatawaliwa na rangi nzuri za wapendanao ambapo ukiachana na listi hiyo mpya iliyoongezeka, mkali wa Bongo Fleva, Dulayo pamoja na wakali kutoka pande za Uganda, Jose Ruffman na Bless Man watakamua nyimbo kali za kimapenzi.
“Muziki mzuri wa kuchombeza malovee utapigwa na DJ, Dulayo naye atasababisha ngoma zake kwa steji bila kuwasahau wakali wa Uganda, Jose Ruffman na Bless Man ambao wameahidi kushusha shoo kali,” alisema Maloto na kuongeza:
“Kutakuwa na sehemu maalumu ya kupiga picha za kumbukumbu kwa wapendanao ambapo pia ‘kapo’ itakayopendeza kuliko zote, itapewa zawadi maalum na uongozi wa ukumbi.”
Katika kuwaandaa wapendanao ambao watapenda kuondoka na zawadi, Maloto amesema ni vyema wahusika wakazingatia mavazi maalum yaliyopendekezwa na waratibu.
“Dress code yetu itakuwa ni rangi ya krimu kwa wanaume na nyekundu kwa wanawake. Nawasihi watu wote wafike kwa wingi kujiwekea historia hii kubwa ambayo haijawahi kutokea,” alisema Maloto.

No comments:

Post a Comment