NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Thursday, February 14, 2013

SHAMSA FORD: NILIPOAMBIWA NIMEJIFUNGUA MWANAUME,NIKALIA!

Na: Imelda Mtema
Niaje mpenzi msomaji wangu? Kama ilivyo kawaida ya safu hii, inakukutanisha na mastaa mbalimbali ambao wamejaliwa kupata watoto na kuongea kuhusu masuala ya familia.
Leo tunaye nyota wa kike wa filamu za kibongo,  Shamsa Ford. Mwigizaji huyu ana mtoto wa miezi kumi anayeitwa Terry ambapo anasema ndiyo roho yake, anampenda balaa! Ungana nami katika mahojiano ambayo nilifanya naye nyumbani kwake Sinza, jijini Dar:
Amani: Mambo Shamsa?
Shamsa: Nzuri, karibu sana.
Amani: Mbona umenawiri hivyo, ni ulezi tu?
Shamsa: Mambo ya saluni haya, si unajua mwanamke urembo!
Amani: Kweli, namuona Terry amekuwa baba sasa.
Shamsa: Mwenzangu maana hapa unavyotuona, vitu vya kuvunjika inabidi tuvihamishe manaa ni mtundu balaa.
Amani: Unajisikiaje unavyomuona amekuwa hivi?
Shamsa: Dah! Kiukweli siwezi hata kuelezea furaha yangu. Nafurahi sana kuitwa mama.
Amani: Niambie ulijisikiaje siku ya kwanza pale ‘Leba’ ulipoambiwa umepata mtoto wa kiume?
Shamsa: Jamani sikuweza kusema zaidi ya kulia tu yaani huyu mtoto aliniliza sana.
Amani: Kwa nini sasa?
Shamsa: Ni furaha tu maana nilikuwa nikimuomba Mungu siku zote, mtoto wangu wa kwanza awe wa kiume.
Amani: Kwa kipindi kirefu ulipotea, je ilisababishwa na ulezi nini?
Shamsa: Kweli, niliamua kumlea mtoto wangu kwanza lakini kwa hivi sasa nimerudi upya kwenye sanaa.
Amani: Kutokana na kuzaa, huoni kama utakuwa umeharibu umbo lako?
Shamsa: Hapana, kwani hivi sasa nafanya mazoezi sana na hata ukiniangalia ninalipa kama zamani.
Amani: Ni nani ungependa kumshukuru zaidi kwa ajili ya mtoto wako?
Shamsa: Wa kwanza kabisa ni baba yake na Zamaradi ambaye ndiyo alikuwa na mimi mwanzo hadi mwisho wakati wa kujifungua.
Amani: Nakushukuru sana Shamsa, acha nirudi ofisini nikawajibike.
Shamsa: Karibu tena siku nyingine.

No comments:

Post a Comment