Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
LEJENDARI
katika tasnia ya sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa
kuwa kitumbo ndii, ishu ambayo imeibua maswali tata kwa watu wake wa
karibu huku mwenyewe akichekelea.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti hili,
kwa sasa mwanadashosti huyo ana dalili zote za kuwa na kibendi lakini mwenyewe anafanya siri.
Baada
ya kuzinyaka habari hizo zinazoendelea kushika kasi mitandaoni, Ijumaa
wanahabari wetu walifunga safari hadi ofisini kwa Johari, RJ Production,
Sinza-Mori, jijini Dar lakini hakupatikana ndipo akapigiwa simu ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Ijumaa: Haloo Johari, mambo vipi?
Johari: Poa tu, sijui naongea na nani?
Ijumaa:
Unaongea na waandishi wa gazeti la Ijumaa, tumefika ofisini kwako
haupo, kuna habari kuwa wewe ni mjamzito. Je, ni kweli?
Johari:
(anacheka sana) Mh! (kicheko tena na tena) Hahahaaa (kicheko
tupu)...niko location (mandhari ya kurekodia filamu), nani amekwambia
mimi ni mjamzito?
Ijumaa: Mtu wako wa karibu. Kwani huo ujauzito una muda gani na baba mtoto wako ni nani?
Johari: Jamani watu wabaya, hivi nyiye mnamjua baba yake?
Ijumaa: Hatumjui ndiyo maana tunauliza.
Johari: Jamani kwani nikizaa kuna ubaya gani? Hata hivyo, kuzaa ni jambo la heri, nitakupigia baadaye.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mtamboni Johari hakupiga kama alivyoahidi.
No comments:
Post a Comment