NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

RAY: SIMUOI MAINDA WALA JOHARI

Stori: Imelda Mtema
KATIKA kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuwafutilia mbali wasanii wenzake, Blandina Chagula na Ruth Suka ‘Mainda’ aliowahi kudaiwa kutoka nao kimapenzi, staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi amefunguka kuwa, hatarajii kuoa msanii kwani anaogopa presha.
 Vincent Kigosi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Ray alisema kuwa anajua matatizo ya kuoa staa hivyo ili kuepukana nayo ameamua kuwekeza penzi lake kwa mwanamke anayefanya kazi benki (jina amelihifadhi kwa sasa) akidai kuwa huyo ndiye tulizo la moyo wake.
 
Ruth Suka ‘Mainda’.
“Kaa ukijua kuwa sina mpango wa kumuoa staa yeyote, mwanamke ninayetarajia kumuoa ni mfanyakazi wa benki na mipango yangu ikikamilika nitakueleza kila kitu. Mimi sitaki presha bwana,” alisema Ray.
Blandina Chagula 'Johari'.

No comments:

Post a Comment