NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Monday, February 18, 2013

STEVE ABANWA SKENDO YA KUTAFUNA RAMBIRAMBI, KUTOKA NJE YA NDOA

KAMA ilivyo kawaida ya safu hii, wiki iliyopita tulimweka kati mwigizaji wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo msomaji ulituma maswali yaliyohitaji majibu kutoka kwake, hapa anayajibu kwa ufasaha, SHUKA NAYO...

ELIMU
Nina furaha ya kuona kazi zako lakini pia napenda kufahamu elimu yako na mtazamo wako kwa jamii. Musa Lukwelo, Dodoma, 0712833104
STEVE NYERERE: Asante, nina elimu ya kidato cha nne, mtazamo wangu ni kuwasaidia Watanzania, hususan vijana wenzangu ili kuendeleza nchi yetu na kuongeza vipato vyao.
HISTORIA KWA UFUPI
Nakupongeza sana Steve kwa kazi nzuri, naomba kujua historia yako kwa ufupi, je, umeoa, una umri gani na una watoto wangapi? Mama Junior, Dar, 0717676615
STEVE NYERERE: Asante, nina mke na watoto wawili, Lisa na Alex, mengine ni siri yangu.
UBAGUZI
Kaka najua upo Bongo Movie Unity, sijui matarajio yenu mnataka muweje ila kwa muonekano wa nje mmejibagua wale mnaojiona mpo juu kuliko wenzenu, badilika kaka kumbuka mpanda ngazi hushuka, sipendi mashauzi yenu, nasikia una cheo pale! Cheo ni dhamana ndugu hukumbuki ulivyosota kabla? Kwa sasa jamii imeashaanza kuichoka kruu yenu, jichanganye na wale unaowaona si  lolote kwako. Baba Lily, Dodoma, 0717720023
STEVE NYERERE: Asante kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.
KUCHAKACHUA RAMBIRAMBI
Nakupongeza kwa kazi nzuri ya kuielimisha jamii, hivi ni kweli huwa una tabia ya kuchakachua fedha za rambirambi? Gasto Luhunga, Tabora, 0754362412
STEVE NYERERE: Kila mtu anayefanya mazuri hategemei kulipwa mazuri zaidi ya kutukanwa na kudharauliwa.
KASOMEA KUIGIZA?
Hivi hiyo kazi uliisomea au kipaji tu? Dulla, Morogoro, 0654283038
STEVE NYERERE: Ni Mwenyezi Mungu amenijalia kipaji hiki, namshukuru.
MIGOGORO BONGO MOVIE
Hivi ni kweli Bongo Movie kuna migogoro, je, unafikiri chanzo ni nini? Elia, Iringa, 0718085308
STEVE NYERERE: Penye wengi hapakosi migongano na siku zote ili kitu kiimarike lazima migogoro iwepo.
KUTOKA NA UWOYA
Steve wewe ni bonge la staa katika tasnia ya filamu, eti ni kweli una uhusiano wa kimapenzi na (Irene) Uwoya? N. Man, Tanga, 0758900144
STEVE NYERERE: Hakuna kitu kama hicho.
USHAURI
Nafurahi sana kaka Steve kwa uigizaji wako maana unavaa uhalisia hasa ile filamu ya Baba Nyerere, nakuomba msiwe mnatoa filamu za mapenzi tu jaribuni kuigiza hata matukio ya jamii na kuwasaidia wasiojiweza. Mwaipopo, 0653317354
STEVE NYERERE: Nashukuru, asante sana.
NJE YA NDOA
Steve nawafahamu watoto wako wawili uliozaa nje ya ndoa, je, unawatunza? Cathy, Dar, 0758570870
STEVE NYERERE: Walete hao watoto kama unawajua.

KUIGA MAISHA YA RAY
Steven nakushauri usipende kujifanya maisha yako ni ya juu kwa kumuiga Ray (Vincent Kigosi), ishi kama ulivyo na usiwe kuwadi wa kuwatafutia mapedeshee wanawake, ipo siku watakugeukia wewe. Frank David, Dodoma, 0715360316
STEVE NYERERE: Asante.

No comments:

Post a Comment