NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

MESSI KUMALIZIA SOKA LAKE ARGENTINA.


MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amedokeza kuwa anaweza kumalizia soka nchini Argentina baada ya kuongeza mkataba na Barcelona ambao utaishia June 2018. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, alifanikiwa kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi mpaka kufikisha mabao 91 mwaka jana kwa klabu na nchi yake. Akizungumza na tovuti ya klabu hiyo Messi amesisitiza kuwa alikuwa akitaka kumalizia soka barani Ulaya akiwa na Barcelona na hajafikiria kwenda katika klabu yoyote barani humo pindi mkataba wake utapokwisha. Messi alisaini mkataba wake mpya Alhamisi mchana na kuwafuata beki wa timu hiyo Carles Puyol na Xavi Hernandez ambao wote waliongeza mikataba yao mwezi uliopita ambayo itawaweka Camp Nou mpaka 2016. Shughuli za utiaji saini mkataba huo mpya zilihudhuriwa na rais wa Barcelona Sandro Rossel, makamu wa rais Josep Maria Bartomeu na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Andoni Zubizarreta.

No comments:

Post a Comment