Stori: Imelda Mtema
Inauma
sana! Imeelezwa kuwa msoto wa mateso aliyopitia kijana Isaack Banda,
raia wa Malawi ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani na bustani (house and
shamba boy), aliyedaiwa kuchomwa moto na mwajiri wake hadi kusababisha
kifo chake, yalikuwa makuu, Risasi Jumamosi limenyetishiwa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea wiki iliyopita nyumbani kwa mwajiri wake huyo maeneo ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Ilifahamika kuwa chanzo cha kukutwa na mateso hayo ya kutisha hadi
kifo, mwajiri wake alimtuhumu kumwibia mali zenye thamani ya dola za
Kimarekani 50,000 (zaidi ya Sh. milioni 80), zilizokuwa ndani ya nyumba
aliyokuwa akilinda na kuitunza iliyopo Kinondoni, Dar.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu waliozungumza na gazeti hili, kijana
huyo alikuwa na takribani miaka miwili akifanya kazi kwa mwanamke huyo
ambaye pia ana uraia wa Marekani.
Kuna madai kuwa baada ya kumtuhumu kwa wizi, kijana huyo alifungwa
kamba ili asifurukute, akapokea kikombe cha mateso kabla ya kuchomwa
moto na kubaki na majeraha ambayo yalisababisha kifo chake akiwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Ndugu hao walidai kuwa huku jamaa akijitetea kwa namna zote kuwa
hajui chochote juu ya upotevu mali hizo, watesaji hawakumsikiliza pamoja
na kwamba aliwaeleza kuwa ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na ndugu
wengine na mshirika wa kibiashara wa mwajiri huyo, mwenye asili ya Asia,
ambao nao walipaswa kubanwa.
Walidai katika hali ya kusikitisha zaidi, watesaji hawakutaka
kumsikiliza hadi walipoona ana hali mbaya ndipo wakamtelekeza kabla ya
kuchukuliwa na wasamaria wema kupelekwa hospitali alikokutwa na umauti.
Juzi Jumatatu, Risasi Jumamosi lilifika katika Makaburi ya
Mwananyamala Kwa Kopa, Dar na ku-shuhudia umati wa waombolezaji wakiwa
katika mazishi ya jamaa huyo huku kila kona makaburini hapo ikitawaliwa
na majonzi.
“Kuna vifo lakini hiki cha Banda kinauma zaidi. Jamaa aliteseka sana,” alisema mmoja wa waombolezaji hao.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni,
Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi
hilo linamshikilia mwanamke huyo ili kusaidia uchunguzi wa shauri hilo

No comments:
Post a Comment