NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 8, 2013

UEFA YAPUNGUZA GHARAMA ZA TIKETI ZA FAINALI CHAMPIONS LEAGUE.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limejibu hoja ambayo ilikuwa ikikua kuhusiana na gharama kubwa za kutizama mechi nchi Uingereza kwa kushusha bei ya tiketi za fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa mpaka kufikia paundi 68. UEFA walituhumiwa kuwanyonya mashabiki wakati wa mchezo wa fainali ya michuano hiyo uliochezwa miaka miwili iliyopita ambapo Barcelona iliifunga Manchester United kwa mabao 3-1 kwa kuwalipisha paundi 176 kwa tiketi ya bei rahisi. UEFA ilitangaza kuwa imesikiliza vilio vya mashabiki na kuamua kupunguza bei ya tiketi kwa ajili ya mchezo huo wa fainali utakaochezwa Mei 25 mwaka huu baada ya kupata maoni kutoka kwa mashabiki wa soka sehemu mbalimbali barani Ulaya. Tiketi 13,000 kati ya 59,000 zitakazouzwa ndio zitapata punguzo la bei hizo mpya lakini zilizobakia zote zitauzwa kwa gharama za juu zitakazoanzia paundi 140 mpaka 330.

No comments:

Post a Comment