NEMAYAN

NEMAYAN

ROBERT

  • THE HOODS SPICK

Friday, February 22, 2013

KUHUSU MWANAFUNZI ALIEJIUA BAADA YA MATOKEO YA FORM IV, NA UJUMBE ALIOACHA VIKO HAPA


Tabora.
Ni kifo ambacho kimetokana na mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kanyenye Tabora Michael Fidelis kutofurahishwa na matokeo yake ya kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu.
Kaka wa marehemu amesema “tangu jana saa 11 marehemu alikua hai kuna mwanafunzi mwingine yuko Mbeya akampigia simu kwamba akaangalie matokeo yametoka ilikua saa 11 jioni, kukuta matokeo mabaya hakurudi nyumbani akaenda anapolala ambako alipangiwa chumba kwa ajili ya kujisomea karibu na nyumbani na kuamua kuchukua uamuzi kama huu, ilikua saa tatu usiku na tumekuja kugundua saa nne baada ya yeye na mwenzake kutotokea nyumbani kuja kula”
Ameendelea kwa kusema “alijinyonga kwa kamba ya manila, ujumbe alioacha ulikua unaishilizia ukisema… mama mimi nakupenda, nimejinyonga kwa sababu matokeo ya form four sio mazuri…… mpaka sasa mwili wa marehemu umeenda kuzikwa kijijini”
Kwenye sentensi hii namkariri rafiki wa marehemu akisema “tulianza nae wote form one pale Kanyenye mpaka form IV, alikua anajitahidi sana kwenye masomo tulikua tunakwenda nae hata tution, darasani alikua mzuri tu tumeenda nae hivyo hivyo mpaka tukafanya mtihani wa form II tukafaulu wote mpaka Mock ya form IV akaja akafanya vizuri, alikua hana vurugu kwa walimu na kuhusu matokeo yalivyotoka mchana alikua kwa mama yake pale anafanya kazi, alikua anaonekana kama mtu ambae hajaelewa matokeo kwani alivyofanya mtihani alikua ana uhakika kabisa kwamba anafaulu lakini matokeo yalivyotoka yalikua tofauti kabisa”

No comments:

Post a Comment